Tuesday 19 November 2013

WIVU WASADIKIKA KUWA SABABU YA KUUA NA KUJIUA KWA RISASI HUKO BUNGONI, ILALA-DAR

Hili ndilo gari walilokuwa wamepanda wahanga wa tukio hilo, Toyota Hilux Surf.
Muonekano wa nyuma wa gari hilo.
Damu zikiwa zimetapakaa eneo la tukio.
Mtu anae daiwa kuwa ni Mfanyabiashar wa jijini Mwanza, na kufahamika kwa jina la Gabriel Munisi amejiua baada ya kushambulia watu wanne kwa risasi asubuhi ya leo eneo la Ilala Bungoni jirani na Klabu ya Wazee.

Shambulizi hilo linaelezwa kuwa ni la kimapenzi limefanywa na Munisi baada ya kuabini nyendo za ndivyo sivyo kwa mpenzi wake aliyetajwa kwa jina la Christina Nando.

Imeelezwa kuwa Mtu huyo aliwashambulia kwa risasi wakiwa ndani ya gari wakitoka ndani hivyo kumpiga risasi dereva wa gari hilo, Francis Samwel, Christina Nando na watu wengine wawili waliokuwapo ndani ya gari hilo ambapo mmoja ni 
 mama mzazi wa Christina.

Taarifa zaidi kuhusu lilivyotokea tukio hilo zinasema, mapema leo asubuhi milio ya risasi zaidi ya kumi ilisikika eneo la Ilala Bungoni karibu na baa maarufu ya Wazee (Club ya Wazee), watu watatu wakiripotiwa kufariki kutokana na tukio hilo linaloelezwa kuwa limetokana na wivu wa kimapenzi.
  
Dereva mmoja wa taxi kituo cha Bungoni ambaye alikuwa shuhuda wa kwanza, alisema mapema leo asubuhi alipata mteja aliyehitaji kupelekwa sehemu, ila kabla hawajafika huko walipokuwa wanataka kwenda jamaa ambaye ndiye alikuwa ni  muuwaji alimuomba akatishe safari na kumtaka ampeleke sehemu nyingine.
  
Dereva  huyo  aliendelea kusimulia  kuwa  alimpeleka jamaa mpaka aneo la tukio hilo kwenye nyumba iliyopo pembeni mwa Hotel mpya iitwayo MM.
  
Mara baada ya kufika hapo, jamaa alitoa sh. 5,000 na kumkabidhi dereva ila cha kushangaza ni kitendo cha jamaa huyo kutoa bastola wakati akiwa anaelekea kwenye geti la nyumba.
  
Wakati jamaa anaelekea getini mlango ulifunguliwa na gari aina ya Toyota Surf ilitoka ikiwa na watu wanne ndani, mwanaume mmoja ambaye alikuwa akiendesha gari , mama mmoja na wadada wawili.

Jamaa akiwa na bastola alianza kuwashambulia watu waliokuwa ndani ya gari hilo na kumpiga risasi dereva na mdada mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Carol... Baada  ya  dreva  taxi  kuona  hali  imechafuka  ilimbidi  akimbie.
  
Vyanzo vingine vinaeleza kuwa katika tukio hilo jamaa pia alimpiga risasi ya mgongoni mama wa mwanamke aliyemuua na pia alimpiga msichana mwingine risasi ya mguu.
  
Mtuhumiwa na dereva aliyekuwa akiendesha gari walifariki palepale huku msichana mmoja akielezwa kufariki akiwa njiani kuelekea hospitali.
  
Bado haijafahamika moja kwa moja chanzo cha mauaji hayo licha ya watu wengi kudai  kuwa  ni  wivu  wa  mapenzi. 

--- Habari kwa mujibu wa blogu za PaparaziHuru na Father Kidevu na GPL




No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...