Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Warioba akimkabidhi Rais Jakaya Kikwete (kulia) Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya leo.
Jaji Warioba akimkabidhi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.AliMohamed Shein (kushoto) Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya leo.
Rais Jakaya Kikwete (kulia) akiteta jambo na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Warioba.
Bendi ya polisi ikitumbuiza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar..
Spika wa Bunge, Anne Makinda (kulia) akisalimiana na mmoja wa waalikwa.
Msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi (kushoto) akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Francis Mbatia (katikati) na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba (kulia).
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Warioba leo amekabidhi Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika hafla fupi iliyofanyika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Hafla hiyo imehudhuria na viongozi mbalimbali wakiwemo wa vyama vya siasa, mawaziri, wabunge na baadhi ya wananchi walioalikwa.
Mheshimiwa Rais Kikwete ameagiza Rasimu hiyo ya Pili ya Katiba Mpya isambazwe kwenye mitandao ili kila Mtanzania aweze kuipata.
(PICHA ZOTE NA HARUNI SANCHAWA / GPL)
No comments:
Post a Comment