Saturday, 13 September 2014

MADA YA SIKU: URAIA PACHA

Swala la uraia pacha limetawala bunge maalumu la katiba. Wajumbe mbalimbali wa bunge hilo  wamekuwa wakitoa mawazo yao kuhusu uraia pacha.Wako wanaoona kuwa uraia pacha hauna madhara na wapo wanaopingana na dhana hiyo.
Kwa upande wangu sioni tatizo lolote kwani Tanzania itakuwa si nchi ya kwanza kuwa na uraia pacha.Kuna chini nyingi tu duniani, zikiwemo zile za Afrika ambazo zimeruhusu uraia pacha na hatujaona tatizo lolote.
Baadhi ya nchi za Afrika ambazo zinaruhusu uraia pacha ni Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Namibia,Nigeria, Lesotho, Sierra Leone, Togo,Afrika ya Kusini (kwa kibali maalum kutoka wizara ya mambo ya nje), Ghana(raia mwenye uraia pacha haruhusiwi kushika nafasi za juu za uongozi)n.k.
Kutokana na mageuzi yanayoendelea duniani sisi kama nchi, hatuwezi kujitenga na mabadiliko haya.Vinginevyo wakati wenzetu wanakimbia,sisi tutakuwa tunatembea.
Kama kuna wasiwasi juu ya uraia pacha tunaweza kuweka vipengele ambavyo vitasaidia kuzuia vitu vinavyoonekana ni hatari mfano kama walivyofanya Ghana kuzuia mtu mwenye urai pacha kushika nafasi za juu za uongozi. Wanaweza vilevile kubana umiliki wa ardhi kwa mtu mwenye uraia pacha ambaye si mzawa n.k
Je kwako wewe msomaji uraia pacha ni hatari kwa taifa?Kama ndivyo hatari hizo ni zipi?Toa mawazo yako na tutayaweka hapa.

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...