Sunday, 9 November 2014

KALI YA SIKU!

Mnyakyusa mmoja aliwaalika watu katika mazishi ya mama yake. Baada ya kushusha jeneza wakatia ndani ya kaburi viazi, mchele na kuku kadhaa. Mhaya mmoja akauliza, 'Vya nini hivyo?'
Akaambiwa, 'Wafu huenda safari ndefu sana, hivi atakula njiani'.
Mhaya akazama kwenye wallet, akatoa laki 2, akaidondoshea akisema, 'vikiisha hivyo atanunua vingine'. Mkurya mmoja akadondoshea laki moja akasema, 'Isipotosha ataongezea hii'
Mchaga akatoa cheque book, akaandika cheki ya laki 5, akachukua ile laki 3 kwenye kaburi na kuacha cheki akisema, 'bora ukachukue hela mbele ya safari kwa cheki. Vibaka wasijeWAKAKUUA bure'.
Shikamoo wachaga!

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...