Friday 27 March 2015

TEMBEA UONE: ANAYEKUTWA NA NGOZI NDIYE ALIYEIBA MBUZI!


                   
Tupo njiani tukielekea Wilaya ya Pangani,mkoani Tanga. Baada ya kupita eneo la Duga, mbele kidogo, tunakuta kundi kubwa la watu wakiwa wamekusanyika.


Palikuwa na zogo kubwa.Dereva tuliekuwa nae alisimama na kuuliza nini kilikuwa kinaendelea. Mmoja ya watu aliyekuwepo katika mkusanyiko ule akamjibu kuwa kuna wezi wa mbuzi wamekamatwa. Tulipoangalia vizuri tukaona kuna watu wawili wamekalishwa chini huku wakiwa na damu nyingi.
Inasemekana watuhumiwa hao walikutwa na ngozi mbichi yenye rangi ya mbuzi aliyepotea hivyo kupelekea kushukiwa kuwa wao ndiyo walikuwa wezi kwani ”anayekutwa na ngozi, ndiye aliyeiba mbuzi”!

KWELI TEMBEA UONE.

Mwandishi Anna Nindi

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...