Picha: GPL
Mvua
zinazonyesha kwasasa nchini hususan jijini Dar zimeleta madhara mengi kubwa
likiwa ni mafuriko.Mbali ya kuwa sababu kubwa ni wakazi waliojenga katika
maeneo yasiyostahili,yakiwemo katika mikondo ya maji, kuna uzembe mwingine
mkubwa pia.Uzembe huu ni mitaro ya kupitisha maji ambayo imeziba.
Kuziba kwa
mitaro kwa upande mmoja ni uzembe wa
wananchi,ambao kwa upande wao hutupa takataka ovyo,katika maeneo yasiyo rasmi.
Kwa upande wa pili ni wahusika na uangalizi wa mitaro hiyo na wale
walioitengeneza(sijui ni halmashauri ya jiji au nani).Kwanini basi?
Sababu ni
hii; mitaro mingi haijazibwa iko wazi tu.Sidhani kama mitaro ya kupitisha maji
inatakiwa kuwa hivi.Kwa kuiacha wazi ndiyo kunachangia wananchi kujitupia ovyo
tu takataka.Athari hizi hazionekani wakati wa kiangazi bali ndiyo haya
tunayoyaona nyakati za mvua.Kwa mtazamo wangu, ni kosa vilevile kwa wahusika
kuanza kusafisha mitaro wakati mvua zikiwa zimeshaanza.Walikuwa wapi kabla?
Kila mtu
awajibike katika eneo /jukumu lake na haya hayatatokea.Ni hayo tu!
Wewe mdau
una lipi la kuchangia?
No comments:
Post a Comment