Thursday, 25 June 2015

HONGERA MILLEN MAGESE KWA TUZO ZA BET!



Tuna kila sababu ya kumpongeza mlimbwende wetu kutoka Tanzania kwa tuzo hizi za BET. Hii inaonyesha wazi kuwa harakati zake  zinatambulika na dunia.
Linapokuja swala linalohusu kuweka Taifa katika ramani hatuna budi wote kujivunia utanzania wetu kwa kumwagia pongezi yule ambaye amesababisha kupeperusha bendera yetu.
Tumpe ushirikiano wa kutosha Millen katika harakati zake hizi za kupambana na endometriosis.

Hongera sana Millen na tunayo fahari kujivunia wewe!