Hospitali moja mjini Stockholm nchini Sweden inatarajiwa kufungua kliniki ya kwanza ya wanaume waliobakwa.
Hospitali
ya South General Hospital tayari ina eneo linalotoa huduma ya dharura
kwa wanawake waliobakwa ama kunyanyaswa kijinsia.Lakini sasa imetangaza siku ya jumatano kuwa itaanza kuwalaza wavulana na wanaume kuanzia mwezi Octoba.
Takriban visa 370 vya unyanyasaji wa kijinsia miongoni mwa wanaume na wavulana viliripotiwa nchini Sweden mwaka uliopita kulingana na vyombo vya habari nchini humo.
No comments:
Post a Comment