Skip to main content

JARIBU KUWA MBUNIFU KATIKA MITINDO

Ukitaka kufanya jambo lako jaribu kuwa mbunifu wewe mwenyewe.Kukosa kwetu ubunifu ndiyo hupelekea wengi kufanya kitu hichohicho. Si mbaya kupenda kitu kizuri kilichofanywa na mwingine ila inachosha kuangalia kitu kimoja tu kila mahali.Mfano linapokuja swala la arusi si lazima wasimamizi(bridesmaids) wavae nguo za rangi moja.Unaweza ukawa na rangi mbili tofauti.Kama una wasimamizi wanne, wawili wanaweza kuvaa nguo za rangi njano isiyokoza na wawili rangi ya zambarau isiyokoza na ukapata mwonekano mzuri tu.Hali kadhalika si lazima wasimamizi wavae nguo za rangi moja,wanaweza kuvaa nguo zenye maua na wakapendeza pia.Wasimamizi wanaweza wengine kuvaa nguo ndefu na wengine fupi.Vile vile wanaweza kuvaa nguo za rangi tofauti (mismatched) wote wane nab ado wakatokelezea!

Nitaonyesha hapa chini jinsi wasimamizi wanavyoweza kuvaa na kupendeza.Tujaribu kuwa wabunifu katika kila tunalofanya!15 Fantastic Floral Bridesmaid Dresses Ideal For An Ultra-Romantic Wedding
Wasimamizi wakiwa na nguo za mauaToday's Bride and Formal Wear- Sorella Vita bridesmaids dresses- Strapless, ombre, sweetheart neckline and chiffon. Perfect for a beach wedding!
Wasimazi wenye nguo ndefu na fupi
Blue Bridesmaids / Emily Wren Wedding Photography
Mchanganyiko wa wasimamizi wenye nguo za rangi moja na maua

Bridesmaids in pretty red dresses
Wasimamizi wakiwa na nguo za rangi moja
Jenny Yoo Annabelle Dress in Shades of Blue! http://jennyyoo.com/nabi05.html
Wasimamizi waliovaa nguo za mchanganyiko

Popular posts from this blog

YEBOYEBO,MTINDO WA NYWELE UNAOPENDWA HADI SASA

MICHORO MBALIMBALI YA HINA

JINSI YA KUPAKA RANGI NDANI YA NYUMBA YAKO

Swala la kuchagua rangi inayofaa ndani ya nyumba huwachanganya wengi.Wengi hushindwa kuamua ni rangi gani wapake. Na endapo mtu atataka kuchanganya rangi za aina mbili au zaidi ni rangi gani atumie? Habari hii inaweza kuwasaidia kidogo kwani nitawawekea baadhi ya picha jinsi rangi zinavyoweza kupangiliwa na kupendeza.Kikubwa vilevile zingatia samani ulizonazo au unazohitaji kuweka katika nyumba yake ili usilete mchanganyiko wa rangi utakaoumiza kichwa.