Friday, 17 July 2015

TANZIA: MSANII BANZA STONE (RAMADHANI MASANJA) AFARIKI DUNIA

Banza stone, enzi za uhai wake

Staa wa Muziki wa Dansi Bongo, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’ amefariki dunia mchana huu baada ya kuugua kwa muda mrefu. Kaka wa marehemu aitwaye Hamis amethibisha msiba huo.
Kwa mujibu wa ndugu wa marehemu, Banza alikuwa anasumbuliwa na fangasi waliokuwa wanamshambulia kichwani (ubongo) na shingoni.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN
CHANZO: GPL