Monday, 21 September 2015

KWA MARA YA KWANZA TIFFAH LIVE!

Staa wa Bongo Fleva,  Nasibu Abdul ‘Diamond’ na mzazi mwenzake Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’ wakimtoa mtoto wao, Latiffah Nasibu 'Princes Tiffah'.
  • Sherehe yake ya 40 usipime, Zari, Diamond waandika historia
Na waandishi wetu
YAMETIMIA! Baada ya kutoonekana sura kwa zaidi ya siku 40 tangu azaliwe, hatimaye mtoto wa mkali wao ndani ya Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Latifah ‘Tiffah’ ameonekana hadharani (live), Ijumaa Wikienda linakuwa la kwanza kuripoti.Diamond na Tiffah

Tukio hilo la kihistoria kwa Diamond na mzazi mwenzake Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’ lilichukua nafasi jana, nyumbani kwake Madale-Tegeta jijini Dar. Waandishi wetu, Musa Mateja na Imelda Mtema waliokuwepo kwenye tukio hilo mwanzo-mwisho waliripoti live Makao Makuu ya gazeti hili, Bamaga-Mwenge.

CHANZO: GPL