Sunday, 11 October 2015

KERO: UJUAJI HUHARIBU MAISHA YA WENGI

Leo tuzungumzie swala la mtu kujiona unajua kila kitu. Ikumbukwe maisha ni safari na vilevile ni darasa. Hata uwe na elimu gani huwezi kujua kila kitu hivyo inatakiwa uwe na utayari wa kujifunza kila siku. Ukiangalia wengi kati ya watu waliofanikiwa kimaisha wamekuwa na utayari wa kujifunza. Na wale wasiotaka kujifunza kwa kuona kuwa wanajua kila kitu huwa hawaendi popote ki maisha.


Mfano,unaweza ikiwa unajua kupika wali wa mbogamboga, akatokea mpishi mwingine na kukuambia kuwa yeye angependa kwa siku hiyo kutengeneza hicho chakula, Kwa mtu muungwana na anaependa kuongeza kitu kingine kichwani mwake atamkubalia mara moja. Ila kwa wale wenzangu na mimi wasiotaka kuonekana kuwa hawajui atakataa kuwa yeye anajua kutengeneza wali huo wa mboga.
Hili ni kosa kubwa sana.Kwani utakuwa umekosa nafasi adimu ya kuongeza ujuzi.
Ukitaka maendeleo kubali kukosolewa. Hii ndiyo siri kubwa ya mafanikio.Huwezi kuwa unajua kila kitu-HAIWEZEKANI.
Na kama unajua kitu vilevile usiwe mchoyo kuwapa ujuzi wako watu wengine. Kwani maisha ni kutoa na kupokea.

MWENYE MASIKIO NA ASIKIE