Friday, 5 February 2016

JIKONI: SANDWICH CAKEMAHITAJI

3 mikate ambayo ipo sliced
     3 Kopo Samaki aina ya tuna
     1 leek
     10 ml sour cream
     1 kopo  mayonnaise
     15 mayai ya kuchemsha
     1 tango
     6 nyanya
     1buch lettuce
     400-500 g kamba
     Limao na  pilipili


JINSI YA KUTAYARISHA

·         Ondoa kingo za vipande vya mkate, hifadhi katika mfuko wa nylon

·         Changanya sour cream, mayonaise na leek, Weka pilipili na limao kupata ladha
·        

    Panga vipande vya mkate katika sinia kubwa kwa mstari kama picha inavyoonyesha hapa chini.
·        


  •    Mwaga mchanganyiko wa sour cream juu ya mikate. Inatakiwa uwe na safu 4 za mkate na 3 za mchanganyiko wa sour cream
  • ·  Juu  ya safuya mwisho ya mikate weka mayonnaise kidogo ili kushikilia garnish
  • ·  Juu ya keki weka slesi za mayai
  • ·    Pamba kwa saladi ( nyanya na tango) kuzunguka keki yako.
  • Mwagia kamba wako juu kabisa. Nyunyiza pilipili na limao