Skip to main content

KIJANA ALIYETOBOLEWA MACHO BUGURUNI AMSIMULIA RC MAKONDA ILIVYOKUWA

Kama kuna kitu kimenishangaza
na kunisikitisha ni huu ukatili na unyama aliofanyiwa kijana huyu Said. Kweli
machozi yamenitoka.
Sikuamini kuwa mtu anaweza
kumfanyia mtu mwingine ukatili wa namna hii.Kilichonisikitisha ni kuona kuwa
Said alishambuliwa mbele ya watu ambao walishindwa kumpa msaada wowote licha ya
Said kupiga kelele za kuomba msaada.
Haingii akilini mtu
anamshambulia mwananchi mwenzie kwa kumchoma visu anavyotaka huku watu wanaona
na wanaendelea na shughuli zao.Na sidhani kama hao wauza kuku hawamjui huyo
mtuhumiwa.


Mimi nawachukulia wote
waliokuwa eneo hilo wakishuhudia tukio huku wakiendelea na shughuli zao kama
wahalifu pia.
Kama haitoshi, mbali na
mtuhumiwa kumjeruhi vibaya Said kwa kisu,akamtoboa macho yake kabisa.Hivi kweli
tumefikia unyama wa aina hii?Unakwenda kumjeruhi na kumtia kilema cha maisha
mtu asiye na hatia?
Said alikuwa mtafutaji,kwa ajili ya familia yake. Saidi
alikuwa ni tegemeo kwa ndugu zake na watoto wake.Leo hii amefanywa kuwa
tegemezi.
Mimi ingekuwa amri yangu hizo biashara zote zilizopo katika
eneo hilo alilofanyiwa ukatili Said ningezifungia na kuwajumuisha wahusika wote
katika kesi inayomkabili mtuhumiwa. Wao si wanafuga wahalifu.
Tunaiomba mahakama imtendee
haki Said. Mtuhumiwa na wote walioshirikiana nae wapate adhabu inayostahili.
Wananchi wenzangu pamoja na
serikali tumpe Said msaada wa kuikabili changamoto aliyonayo.
KWA JINSI GANI?
Kwanza, kuona kama anaweza
kusaidiwa kurudisha uwezo wake wa kuona.Hapa serikali na wana harakati kufanya utafiti wa haraka kama kuna uwezekano wa kupata tiba hii nje ya
nchi.
Pili,Kama uwezo wa kutibiwa  upo, gharama ziainishwe na watu tumchangie.
Pole sana Said na tupo pamoja
na wewe na nuna uhakika utaipata haki yako na tutasaidia matibabu yako.

Popular posts from this blog

YEBOYEBO,MTINDO WA NYWELE UNAOPENDWA HADI SASA

MICHORO MBALIMBALI YA HINA

JINSI YA KUPAKA RANGI NDANI YA NYUMBA YAKO

Swala la kuchagua rangi inayofaa ndani ya nyumba huwachanganya wengi.Wengi hushindwa kuamua ni rangi gani wapake. Na endapo mtu atataka kuchanganya rangi za aina mbili au zaidi ni rangi gani atumie? Habari hii inaweza kuwasaidia kidogo kwani nitawawekea baadhi ya picha jinsi rangi zinavyoweza kupangiliwa na kupendeza.Kikubwa vilevile zingatia samani ulizonazo au unazohitaji kuweka katika nyumba yake ili usilete mchanganyiko wa rangi utakaoumiza kichwa.