Friday 21 December 2018

SAFARI YANGU YA ZANZIBAR (SPICE ISLAND) Par

Unapoisoma historia ya mji wa Unguja huwezi kuacha  kuzingumzia kanisa la Anglikana,Mkunazini.Habari za kanisa hili nilizisikia muda mrefu sana ila katika safari zangu zote za kwenda Unguja katika Siku za nyuma Siku wapi kupata ushabiki wa  kwenda kutembelea.
Ni asubuhi ya siku ya Jumapili,majira ya saa 5 asubuhi naanza tour ya jiji la Unguja, nikiwa sina ratiba kamili ya wapi ninakwenda kutembelea ,Mwenyeji wangu alishapanga kuhusu hiyo tour na dereva wa kunipeleka. Tulizunguka sehemu nyingi bila ya kuwa na dira. Alinionyesha jengo la baraza  la wawakilishi Zanzibar ambalo ni jengo zuri sana kwa muonekano. Akanionyesha ofisi za Bilozi ndogo mbalimbali.Akanionyesha hospitali ya mnazi mmoja n.k
Tulizunguka kwa miguu mji Mkongwe ambapo zamani makazi ya watu yalikuwa mengi ila cha kushangaza kwasasa ni maduka ya kuuza vitu vya kitalii na migahawa ya vyakula!
Tukaenda Ngome kongwe ambapo kulikuwa na tamasha kubwa la filamu  almaarufu kama Zanzibar International Film Festival(ZIFF).Kulikuwa na watalii wengi kutoka sehemu mbalimbali duniani.
Tulipokuwa hapo tamashani nikamuuliza guide wangu kuhusu kanisa la mkunazini.Akaniambia kuwa halikuwa mbalimbali na pale ila kama nilitaka kuona mengi twende Siku inayofuata kwani leo ni Jumapili na watu wanasali hivyo sitaweza kuona kila kitu.Nilimkubalia.
Siku iliyofuata amvayo ni Jumatatu kati ya saa 5 na 6 mchana Tuliwasili katika kanisa la Mkunazini,lililopo katika barabara ya Mkunazini, mji mkongwe.
Watalii wengi walikuwa wamepanga foleni wakisubiri kulipia kuingia ndani.Watalii wanalipa zaidi ya wazawa na gharama huoongezeka kama unahitaji tour guide.Miki nililipa kwa ajili ya guide pia kwani dereva wangu nilimruhusu akafanye shughuli nyingine na anirudie baada ya masaa  2. Niliongozana na guide wa kike na mara moja akaanza kunieleza lini kanisa lilijengwa na ni kwanini linautwa kanisa la Mkunazini.
Je,unajua kwa nini lilijengwa mahali hapo?Na je,ni nani alichochea ujenzi huo? Na je,lilijengwa kwa muda gani?
Kujua haya yote soma sehemu ya 2 ya Safari yangu ya Zanzibar


Kanisa la Anglikana,Mkunazini






No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...