Ni asubuhi ya siku ya Jumapili,majira ya saa 5 asubuhi naanza tour ya jiji la Unguja, nikiwa sina ratiba kamili ya wapi ninakwenda kutembelea ,Mwenyeji wangu alishapanga kuhusu hiyo tour na dereva wa kunipeleka. Tulizunguka sehemu nyingi bila ya kuwa na dira. Alinionyesha jengo la baraza la wawakilishi Zanzibar ambalo ni jengo zuri sana kwa muonekano. Akanionyesha ofisi za Bilozi ndogo mbalimbali.Akanionyesha hospitali ya mnazi mmoja n.k
Tulizunguka kwa miguu mji Mkongwe ambapo zamani makazi ya watu yalikuwa mengi ila cha kushangaza kwasasa ni maduka ya kuuza vitu vya kitalii na migahawa ya vyakula!
Tulizunguka kwa miguu mji Mkongwe ambapo zamani makazi ya watu yalikuwa mengi ila cha kushangaza kwasasa ni maduka ya kuuza vitu vya kitalii na migahawa ya vyakula!
Tukaenda Ngome kongwe ambapo kulikuwa na tamasha kubwa la filamu almaarufu kama Zanzibar International Film Festival(ZIFF).Kulikuwa na watalii wengi kutoka sehemu mbalimbali duniani.
Tulipokuwa hapo tamashani nikamuuliza guide wangu kuhusu kanisa la mkunazini.Akaniambia kuwa halikuwa mbalimbali na pale ila kama nilitaka kuona mengi twende Siku inayofuata kwani leo ni Jumapili na watu wanasali hivyo sitaweza kuona kila kitu.Nilimkubalia.
Siku iliyofuata amvayo ni Jumatatu kati ya saa 5 na 6 mchana Tuliwasili katika kanisa la Mkunazini,lililopo katika barabara ya Mkunazini, mji mkongwe.
Watalii wengi walikuwa wamepanga foleni wakisubiri kulipia kuingia ndani.Watalii wanalipa zaidi ya wazawa na gharama huoongezeka kama unahitaji tour guide.Miki nililipa kwa ajili ya guide pia kwani dereva wangu nilimruhusu akafanye shughuli nyingine na anirudie baada ya masaa 2. Niliongozana na guide wa kike na mara moja akaanza kunieleza lini kanisa lilijengwa na ni kwanini linautwa kanisa la Mkunazini.
Je,unajua kwa nini lilijengwa mahali hapo?Na je,ni nani alichochea ujenzi huo? Na je,lilijengwa kwa muda gani?
Kujua haya yote soma sehemu ya 2 ya Safari yangu ya Zanzibar

Kanisa la Anglikana,Mkunazini
No comments:
Post a Comment