Monday, 30 September 2013

KIKWETU KWETU NA KHANGA

UREMBO WA HINA

  

Polisi kulinda benki zote Dar

Kamishna Suleiman Kova
Kufuatia kukithiri kwa matukio ya uhalifu  wa  kupora fedha kwenye mabenki jijini Dar es Salaam, kuanzia leo benki zitakuwa zinalindwa na Jeshi la Polisi.

Aidha, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia mtu mmoja mwenye asili ya kiasia, kwa tuhuma za kuhusika katika matukio hayo uliofanyika hivi karibuni.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Kamishna Suleiman Kova, alisema uamuzi wa kulinda benki umefikiwa kufuatia mkutano kati yake na Makamanda wa Polisi wa Mikoa wa Kanda hiyo.

Kamannda Kova alisema wamekubaliana mambo kadhaa ili kuhakikisha uhalifu huo unaofanywa na magenge ya kihalifu unadhibitiwa na kwamba makamanda hao wametakiwa kuhakikisha kuwa wanashiriki kikamilifu katika utekelezaji wake.

Wakati huohuo  Kamanda  Kova alisema Jeshi hilo limefanikiwa kumkamata Azim Chokera (47) kwa tuhuma za kuhusika katika  matukio yote mawili.

La kwanza ni la juzi na lile la mwishoni mwa wiki ambayo mabilioni ya fedha yaliibiwa na watu waliovalia sare za Jeshi la Polisi na Chokera akionekana akiingiza  ndani ya benki hizo na kutoa maelekezo kwa wenzake kwa njia ya simu.

 
CHANZO: NIPASHE

Dada yake Mbowe afariki dunia ajalini

Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe
Dada wa Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, pamoja na mume wake wamefariki dunia huku watu wengine watatu kukijeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupasuka tairi na kupinduka.

Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, Costatine Massawe, alisema kupitia kwa Mkuu wa Upelelezi mkoa huo (RCO), Aziz Kimata, kuwa ajali hiyo ilitokea jana saa 1:30 asubuhi  eneo la Kabuku Wilaya ya Handeni barabara kuu ya Tanga-Chalinze.

Aliwataja waliokufa kuwa ni Grace Aikaeli Mbowe (Dada yake na Mbowe)  na mumewe, Ibrahim Lukindo (52).

Kimata alisema majeruhi wa ajali hiyo ni Ridhiwani Bakari (29) aliyekuwa na mkewe Zeddy Nzuke (29) raia wa Kenya pamoja na mtoto wake mwenye umri wa miaka miwili na miezi minne, Mariam Ridhiwan ambao wamelazwa katika Hospitali ya Magunga wilayani Korogwe.

Alisema walipata ajali hiyo wakati wakitoka jijini Tanga na ghafla gari namba T 277 CAJ aina ya Cresta waliyokuwa wakisafiria ilipasuka tairi la mbele na kupinduka.

Aliongeza kuwa baada ya kupasuka tairi, gari hilo liliingia chini ya daraja na kusababisha vifo na majeruhi.

Muuguzi wa zamu wa Hospitali ya Magunga, Nayela Missingo, alisema alipokea majeruhi watatu na kwamba jitihada za kuwahamishia Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) zinafanyika kwa kuwa hali zao siyo nzuri.

Missingo alisema mtoto Mariam ndiye amejeruhiwa sana katika kichwa na kwamba tangu alipofikishwa hospitaini, hakuwa katika hali nzuri.
CHANZO: NIPASHE

Miss Philippines Megan Young crowned Miss World 2013 in Bali


Megan Young


Miss World Megan Young of the Philippines (28 Sept 2013)Megan Young won ahead of Miss France and Miss Ghana

The 2013 Miss World pageant has been won by Miss Philippines, Megan Young, on the Indonesian island of Bali.
US-born Ms Young, 23, beat 126 other contestants and pledged to be "the best Miss World ever".
The competition was moved to Bali from the capital, Jakarta, because of protests from hardline Muslim groups.
Security for Saturday's event was high in Bali, a resort island with a majority Hindu population, but no further demonstrations were reported.
Miss France, Marine Lorphelin, came second in the contest and Miss Ghana, Carranzar Naa Okailey Shooter, took third place.

NBC YATENGA SIKU MAALUMU KUWASHUKURU WATEJA WAO

01
Meneja wa Benki ya NBC Tawi la MnaziMmoja, Judith Motta (kulia) akitoa maelezo ya huduma mbalimbali za kibenki katika tawi lake kwa mmoja wa wateja wa benki hiyo, ….. katika ‘Siku maalumu ya kuwashukuru Wateja’ ambayo ni sehemu ya maandalizi ya maadhimisho ya Mwezi wa Huduma kwa Wateja wa NBC unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao. Wateja waliwekewa zulia jukundu wakati wakuingia katika tawi hilo, kupata viburudisho wakati wakisubiri kuhudumiwa, walipata nafasi yakupewa maelezo ya huduma za kibenki za NBC na pia  kujibiwa maswali
yao.

J. Martins featuring Dj Arafat - Touchin Body (Official Video)

Sunday, 29 September 2013

WEMA SEPETU, JACOB STEVEN KATIKA TAKE ONE

Swissport wajipanga kudhibiti vitendo vya ugaidi


Kampuni ya kuhudumia ndege, abiria na mizigo Swissport kwa kushirikiana na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini wamejipanga kuzuia ugaidi kuingia nchini.
Mkurugenzi wa Swissport, Gaudency Temu, aliwaambia wanahabari waliofanya ziara katika viwanja mbali mbali vya ndege nchini sambamba na uwekaji wa mashine mpya na za kisasa zilizonunuliwa na Swissport kwa lengo la kupunguza uhalifu nchini.
Katika zirara hiyo baadhi ya wanahabari wameshuhudia mtambo mpya wa kuzuia uhalifu ikifanya kazi kwa kuongezwa na wataalam ambao wamepata mafunzo nchini Israel.
Mkurugenzi msaidizi wa kitengo cha kupakia na kupokea mizigo Swissport Cargo, Oscar Mgina, alisema kutokana na kufungwa kwa mashine mpya na za kisasa katika kitengo hicho, Swissport imekuwa mwiba mkali kwa watu wasio waaminifu ambao wamekuwa wakisafirisha maliasili na madini kinyume na taratibu za mamlaka husika.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

PENDEZESHA NYUMBA YAKO KWA FOUNTAIN

Kama kuna kitu napenda kiwepo katika mazingira ya nyumba angu ni "foutain".Binti afa kwa kumwagiwa maji ya moto na bibi yake

Kisa alichelewesha mwiko wa kusongea ugali
Mtoto mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Zuhura (6), mkazi wa Lulumba, Wilaya ya Iramba mkoani Singida, amefariki dunia baada ya kumwagiwa maji ya moto na bibi yake.
Imedaiwa kuwa bibi huyo, Magreth Sombi (55), alimmwagia mtoto huyo maji ya moto baada ya kuchelewa kumpelekea mwiko wa kusongea ugali aliomtuma.
Akielezea kisa hicho, Mwenyekiti wa mtaa huo, Abel Seth, alisema tukio hilo lilitokea Jumanne iliyopita.
Alisema bibi huyo anadaiwa kumtuma mtoto huyo mwiko na alipochelewa alimmwagiwa mwilini maji ya moto yaliyokuwa yamechemka kwa ajili ya kupikia ugali.
"Kama haikutosha, Magreth kwa ushirikiano na mtoto wake, Naomi walimkamata kwa nguvu Zuhura na kutumbukiza viganja vyake vyote ndani ya sufuria iliyokuwa na maji yaliyochemka...mtoto aliungua sana na nyama zote kutoka..." alisema kwa masikitiko.
Aliongeza kuwa binti huyo alifariki dunia kesho yake (Septemba 25) wakati akipatiwa tiba katika hospitali ya wilaya ya Iramba.

Saturday, 28 September 2013

BREAKING NEWS: Magazeti ya Mtanzania na Mwananchi yafungiwa


 
                                             TAMKO LA SERIKALI

Serikali imeyafungia  kutochapishwa Magazeti ya MWANANCHI na MTANZANIA kuanzia 27 Septemba,2013  kutokana na mwenendo wa magazeti hayo kuandika habari na makala  za uchochezi na uhasama kwa nia ya kusababisha wananchi wakose imani kwa vyombo vya dola hivyo kuhatarisha amani na mshikamano ulipo nchini.

Gazeti la MWANANCHI limefungiwa kutochapishwa kwa siku kumi na nne(14) kuanzia 27 Septemba,2013.Adhabu hii imetangazwa kwa Tangazo la Serikali(Government Notice )Namba 333 la tarehe 27 septemba,2013.

Gazeti la MWANANCHI limepewa adhabu hiyo kutokana na hivi karibuni kuchapisha habari zenye mwelekeo wa uchochezi na uvunjifu wa amani,mfano tarehe 17 Julai,2013 katika toleo Namba 4774 ilichapisha habari isemayo “MISHAHARA MIPYA SERIKALINI 2013”  kwa kuchapisha waraka uliozuiliwa kwa matumizi ya vyombo vya habari waraka huo ulikuwa wa Siri  haukupaswa kuchapishwa Magazetini.

Aidha, katika toleo la Jumamosi,tarehe 17 Agosti,2013 lilichapisha habari yenye kichwa kisemacho “WAISLAM WASALI CHINI YA ULINZI MKALI”  habari hiyo ilikolezwa na picha ya mbwa  mkali mwenye hasira.Habari na picha hiyo ilitoa tafsiri ya kuwa Jeshi la Polisi lilipeleka Mbwa katika maeneo ya ibada ya waumini wa dini ya kiislam.Jambo ambalo halikuwa la  ukweli.

Jeshi la Polisi katika doria siku hiyo halikupeleka mbwa katika maeneo ya Misikiti.Serikali na jeshi la Polisi linaheshimu na kuzingatia maadili ya dini ya Kiislamu na kwa hiyo Jeshi lake haliwezi kupitisha au kuingiza mbwa katika maeneo ya ibada.
Hivyo basi,kwa gazeti hili kuchapisha habari iliyokolezwa na picha ya mbwa ni uchochezi wa kulichonganisha Jeshi la Polisi na waumini wa dini ya kiislam  mbwa ni najisi hapaswi kuingia  katika maeneo ya ibada.

Gazeti la MTANZANIA limefungiwa kutochapishwa kwa siku tisini(90) kuanzia tarehe 27 Septemba,2013 kwa kuchapisha habari zenye uchochezi.Gazeti hili limeonywa mara nyingi  lirekebishe mtindo wake wa uandishi wa  kichochezi na lizingatie maadili na Sheria na Kanuni za  fani ya Habari.
Pamoja na kuonywa gazeti hili halikuonyesha kuzingatia maelekezo ya Msajili wa Magazeti, mfano ;katika toleo na 7262 la 20 Machi,2013 liliandika habari yenye kichwa kisemacho “URAIS WA DAMU”,tarehe 12 Juni,2013,toleo Namba 7344 lilichapisha makala isemayo “MAPINDUZI HAYAEPUKIKI”.
Aidha, siku ya Jumatano,tarehe 18 Septemba,2013 katika toleo Namba 73414 ukurasa wa mbele lilichapisha Kichwa cha habari kisemacho “SERIKALI YANUKA DAMU” taarifa hiyo ilikolezwa na picha zilizo unganishwa kwa ustadi mkubwa kwa kutumia kompyuta  kutapakaza rangi nyekundu mithili ya damu nyingi kumwagika .Katika habari hiyo gazeti hilo limedai bila uthibitisho kuwa Jeshi la Polisi linahusika  na wahanga waliomizwa na watu wasiojulikana kwa kumwagiwa tindikali na  waliyovamiwa na kujeruhiwa vibaya.
Vile vile gazeti hilo limeishtumu serikali kuwa goigoi katika kushughulikia matukio yenye sura ya kigaidi.
Kwa ujumla wake habari hiyo ni ya kichochezi ina lengo la kuwafanya wananchi wavichukie vyombo vya ulinzi na usalama  wavione kuwa haviwasaidii.
Kutokana na makosa yalitajwa hapo juu serikali imelifungia gazeti la Mtanzania  kutochapishwa kwa muda wa siku tisini(90) kwa Tangazo la Serikali Namba 332(Government Notice No.332) la tarehe 27 septemba,201.

Abdul Haji:Mkenya aliyekuwa tayari kuuawa


Abdul Haji akimwokoa mtoto asiuawe na magaidi. Picha ya maktaba 
Wakati vyombo vya usalama vya Kenya vikitangaza kulidhibiti jengo lote la Westgate lililovamiwa na magaidi wanaodaiwa kuwa wa kundi la Al-Shabaab, baadhi ya watu waliojitoa muhanga na kufanikiwa kuokoa maisha ya wengine, wanaendelea kuibuka.
Hivi karibuni gazeti hili lilichapisha habari juu ya askari wa Kikosi Maalumu cha Anga (SAS) cha Uingereza, aliyeweza kuokoa zaidi ya watu 100 ndani ya jengo hilo.
Hivi karibu, baadhi ya vyombo vya habari vya Kenya vimemnukuu pia  Abdul Haji (38) ambaye ni raia wa kawaida aliyeweza kufika ndani ya jingo hilo na kuokoa watu waliokuwa wametekwa na wanamgambo hao wanaodaiwa kuwa wa Al Shabaab.
Gazeti la Daily Nation, limemnukuu kijana huyo akisema alipata ujumbe mfupi wa simu ya mkononi (SMS) kutoka kwa kaka yake ukisomeka kuwa “Nimekwamba Westgate, nadhani kuna magaidi wamevamia hapa, niombee”.
Kijana huyo ambaye asili yake ni Msomali, alisema alipata sana hofu kutokana na ujumbe huo wa kaka yake kwani ilikuwa ni wiki mbili tu tangu televisheni moja ya nchi hiyo kumtaja kaka yake huyo kama mmoja wa watu anaowasaidia magaidi hao wa Al Shabaab.

PENDEZESHA NYUMBA KWA BUSTANI

Garden Piano garden gardening garden decor small garden ideas diy gardening garden ideas garden art diy garden diy darden gardening on a budget creative gardening ideas

Shelf Garden garden gardening garden decor small garden ideas diy gardening garden ideas garden art diy garden diy darden gardening on a budget creative gardening ideas

Ivy, ferns and other tropical plants in a tall white stone pot against a red brick wall.

DREADLOCK HAIR STYLE FOR ALL

Beautifully styled locs / dreadlocks by Naturaleemee

Nubian Princess | Nubian Princess! | Twists, Braids and Dreadlocks Hairstyles

Dread Envy

#dreads #dreadlocks #hair #hairstyle
Dread Envy

Dread Envy

RAIS JAKAYA KIKWETE AKIHUTUBIA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA JANA

MKE WA RAIS MAMA SALMA KIKWETE AZURU NEBRASKA NCHINI MAREKANI

IMG_2914 
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akipokewa na Founder, Benefactor and Chief Executive Officer wa Taasisi ya Opportunity Education Bwana Joe Ricketts kwenye uwanja wa ndege katika mji wa Omaha uliopo katika Jimbo la Nebraska nchini Marekani tarehe 27.9.2013 IMG_2917 
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea ua kutoka kwa binti Kate Stephens, 7, mara baada ya Mama Salma kutua kwenye uwanja wa ndege wa Omaha huko Nebraska nchiniMarekani tarehe 27.9.2013. IMG_2976 
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akionyeshwa na Bwana James Ricketts, President and Chief Operations Officer, wa Taasisi ya Oppoturnity Education shughuli mbalimbali za kununua na kusafirisha vifaa vya elimu kwenda kwenye shule katika nchi mbalimbali hapa duniani ikiwamo Tanzania wakati Mama Salma alipotembelea Taasisi  hiyo yenye Makao Makuu yake huko Omaha katika Jimbo la Nebraska nchini Marekani tarehe 27.9..2013. IMG_2992Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akipokea zawadi ya ngao kutoka kwa Bwana Joe Ricketts, Founder, Benefactor and Chief Executive Officer wa Taasisi ya Opportunity Education iliyoko huko Omaha nchini Marekani. Bwana Ricketts alitoa zawadi hiyo kwa kutambua mchango mkubwa sana alioufanya Mama Salma binafsi na Taasisi yake ya WAMA Foundation katika masuala ya elimu. Afya na uwezeshaji kwa akina mama.

Washtakiwa EPA jela miaka 13


Washtakiwa wa EPA, Bahati Mahenge (kulia), Manase Mwakale (katikati) wakiwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam jana, baada ya kuhukumiwa.Mahenge alihukumiwa kwenda jela miaka saba wakati Mwakale akihukumiwa miaka mitano. Picha na Venance Nestory 
Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu kwenda jela jumla ya miaka 13, washtakiwa watatu katika kesi ya wizi wa Sh1.1 bilioni katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).
Akitoa hukumu hiyo jana kwa niaba ya wenzake, Jaji Sekela Mushi na Sam Rumanyika,Msajili Lameck Mlacha alisema mshtakiwa Bahati Mahenge atatumikia kifungo cha miaka saba jela.
Mshtakiwa Manase Makale atatumikia kifungo cha miaka mitano jela na mkewe ambaye ni mshtakiwa katika kesi hiyo, Edda Makale atatumikia kifungo cha mwaka mmoja na nusu.

Friday, 27 September 2013

MAONYESHO YA UWEKEZAJI KANDA YA KASKAZINI YALIYODHAMINIWA NA NMB YAFANA

photo1
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akipata maelezo kutoka kwa Meneja Mawasiliano wa Benki ya NMB Bi. Josephine Kulwa (kushoto) alipotembelea banda la NMB katika maonesho ya Uwekezaji Kanda ya Kaskazini yaliyofanyika Jijini Tanga 26-27/9/2013. Walioambatana naye ni Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji Mhe. Dr. Mary Nagu, Mkuu wa Mkoa wa Tanga Kapteni Mstaafu Mh. Chiku Galawa, Mwenyekiti wa Mkutano wa Uwekezaji Nd. Salum Shamte pamoja na viongozi na washiriki wengine.photo2Naibu Waziri TAMISEMI Mh. Aggrey Mwanri akisaini kitabu cha wageni baada ya kutembelea banda la NMB katika maonesho hayo. Kutoka kulia ni Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa NMB Bi. Vicky Bishubo, Meneja Mawasiliano wa Benki ya NMB Bi. Josephine Kulwa pamoja na wafanyakazi wa NMB Tawi la Madaraka Tanga.photo3Mkurugenzi Ukaguzi wa ndani wa Makampuni ya Impala Bw. Julius Makara (kushoto) akipewa maelezo ya kuhusu Huduma Mbalimbali za Benki ya NMB toka kwa Meneja Mahusiano Mwandamizi wa Wateja Wakubwa Bw. Nsolo Mlozi baada ya kutembelea banda la NMB

RAIS KIKWETE ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO UBALOZI WA KENYA NEW YORK

0L7C0424Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo kwenye ofisi za ubalozi wa Kenya wa kudumu katika Umoja wa Mataifa jijini New York jana kufuatia shambulizi la kigaidi katika sehemu ya biashara ya West Gate jijini Nairobi Kenya hivi karibuni.Kulia ni Naibu Balozi wa Kenya wa kudumu Umoja wa Mataifa(Deputy Permanent Representative) Mhe.Koki Muli Grignon.0L7C0510Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwafariji wafanyakzi wa Ubalozi wa kudumu wa Kenya katika Umoja wa Kimataifa muda mfupi baada kusaini kitabu cha maombolezo katika ofisi za ubalozi huo jijini New York, Marekani leo mchana kufuatia shambulizi la kigaidi jijini Nairobi ambapo watu kadhaa walipoteza maisha(photos by Freddy Maro)

Kikwete kuipangua Tanesco


Rais Kikwete
New York. Rais Jakaya Kikwete amesema Serikali ina mpango wa kulifumua Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ili likidhi mahitaji ya nchi.
Akizungumza juzi na ujumbe wa Shirika la Millenium Challenge (MCC), ulioongozwa na Daniel Yohannes jijini New York, Rais Kikwete alisema Serikali italifanyia Tanesco mageuzi muhimu na marekebisho makubwa.
Alisema marekebisho hayo yanalenga kuisaidia Serikali kuharakisha jitihada zake kusambaza umeme kwa wananchi wengi zaidi.
Serikali imeliweka suala la usambazaji umeme kwa wananchi mijini na vijijini, miongoni mwa maeneo yake ya vipaumbele.
“Pia, Serikali yetu itaangalia viwango vya malipo vinavyotozwa na Tanesco kwa wateja wake,” alisema Rais Kikwete na kuongeza:
“Mageuzi haya katika Tanesco ni muhimu sana na yameanza kufanyika, hakika Serikali imedhamiria kuyakamilisha mageuzi hayo muda mfupi iwezekanavyo.”

OUTDOOR FOUNTAIN

MITINDO ZAIDI YA DREADLOCK

Dreadlock for Black Womenflat twist for wedding | dreadlock hairstyles for black women Brown colored dreadlock updo ...
Hii style inaweza kutumiwa na mabibi arusipics of colored dred locks | Styled colored adorned Dreadlocks | Flickr - Photo Sharing!

Dreadlock-Hairstyles · ThirstyRoots | Jul 27, 2010 | Comments 0

START YOUR OWN ONLINE BUSINESS

 Many people are working online especially during this time of CoronaYou can do this also if you have a will.  Register for a Free Live Webi...