Sunday 30 June 2013
HABARI KATIKA PICHA:OBAMA AKIWA ROBBEN ISLAND
Gereza la Robben
Rais Obama na mkewe Michelle wakitembea katika gereza la Robben karibu na mji wa Cape town.
MAMA SALMA KIKWETE KWENYE MKUTANO WA SMART PARTNERSHIP 2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na Rais wa Sri Lanka Mheshimiwa Mahinda Rajapaksa wakati wa mkutano wa smart partnership dialogue 2013 unaofanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere hapa Dar es Salaam kuanzia tarehe 28.6.2013.
Rais Jakaya Kikwete akifurahia jambo na Mfalme Mswati wa Swaziland na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Ndugu Benard Membe wakati wa chakula cha usiku kilichoandaliwa na Rais Kikwete kwa Marais na wajumbe wa mkutano wa smart partnership unaofanyika Dar es Salaam kuanzia tarehe 28.6 hadi 30.6.2013.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Mama Salma Kikwete akijiandaa kuzungumza na wake wa Marais na Wakuu wa nchi wakati wa mkutano wa smart partnership tarehe 29.6.2013 kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere hapa Dar es Salaam.
Baadhi ya wake wa viongozi mbalimbali wanaohudhuria mkutano wa smart partnership wakimsikiliza Mama Salma Kikwete (hayupo pichani) wakati akizungumza nao kwenye ukumbi wa Mwalimu Nerere tarehe 29.6.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa pamoja na Mke wa Mfalme wa Mswati wa Swaziland, Inkhosikati Lambikiza (kushoto), na Mwakilishi wa Mke wa Rais Joseph Kabila wa DR Congo (kulia) wakimwalika Mke wa Makamu wa Rais wa Zambia Mama Charlotte Scott (hayupo pichani) kujiunga nao katika picha ya pamoja mara baada ya kikao chao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere tarehe 29.6.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wake wa Marais na Wakuu wa nchi wanaohudhuria mkutano wa smart partnership unaofanyika hapa Dar es Salaam. Kutoka kushoto no Mama Charlotte Scott, Mke wa Makamu wa Rais wa Zambia akifuatiwa Inkhosikati Lambikiza, Mke wa King Mswati, Mama Salma Kikwete, akifuatiwa na Mama Siti Hasma, Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu wa Malaysia Mahathir Mohammed na kulia ni mwakilishi wa Mke wa Rais wa DR Congo.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiaagana na Mama Siti Hasma mara baada ya kuhudhuria kikao cha wake wa marais na wakuu wa nchi kwenye mkutano wa smart partnership.
Mke wa Rais akiwa katika picha ya pamoja na Inkhosikati Lambikiza wa Swaziland.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiagana na Mama Charlotte Scott
Mama Salma Kikwete na Inkhosikati Lambizana wakijiandaa kwenda katika chakula cha usiku kilichoandaliwa kwenye ukumbi wa mkutano wa Mwalimu Nyerere.
Waziri Mkuu wa Malaysia Mheshimiwa Najib Razak akiwa pamoja na Mama Salma Kikwete na Inkhosikati Lambizana wakimwangalia simba dume aliyewekwa nje ya ukumbi wa jengo la mikutano la Mwalimu Nyerere baada ya viongozi hao kuhudhuria chakula cha usiku tarehe 29.6.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiaagana na Mfalme Mswati wa Swaziland mara baada ya chakula cha usiku.
Rais Jakaya Kikwete akiiagana na Waziri Mkuu wa Malaysia Mheshimiwa Najib Razak mara baada ya viongozi hao kupata chakula cha usiku kwenye ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere tarehe 29.6.2013.
PICHA NA JOHN LUKUWI
OBAMA...OBAMA
Kutua Dar kesho... Jiji lazizima mabango ya kumkaribisha kila kona
Ulinzi wazidi kuimarishwa, askari wa JWTZ wahusika
Hekaheka zimetanda jijini Dar es Salaam,ikiwa ni zaidi ya saa 24 kabla ya kuwasili kwa Rais Barack Obama.
Rais Obama, atawasili nchini kesho akitokea Afrika Kusini, ambapo pamoja na mambo mengine, alizungumza katika mkutano wa ‘viongozi vijana wa Afrika’ na kujibu maswali kutoka nchi tofauti.
Mkutano huo ulifanyika jana jioni huko Soweto nchini Afrika Kusini, ambapo alipokewaa na kujibu maswali kutoka Kenya, Uganda, Nigeria na Afrika Kusini kwenyewe.
Jijini Dar es Salaam, shughuli kadhaa zikiwamo za ulinzi na usalama, zinafanyika kwa kasi na umakini kuhakikisha ziara ya Rais Obama inafanyika pasipo bughudha. kujibu maswali kutoka Kenya, Uganda, Nigeria na Afrika Kusini kwenyewe.
Jijini Dar es Salaam, shughuli kadhaa zikiwamo za ulinzi na usalama, zinafanyika kwa kasi na umakini kuhakikisha ziara ya Rais Obama inafanyika pasipo bughudha.
Hata hivyo, sehemu kubwa inayohusu masuala ya itifaki, ulinzi na usalama yanafanywa na taasisi za Marekani, kwa kuzishirikisha taasisi za ndani kwa kiwango kidogo.
“Hawa jamaa (Wamarekani) wanapoingia nchi yeyote wakiwa na Rais wao, shughuli nyingi na uamuzi wanafanya wao, sisi wa ndani inakuwa kushirikishwa kwa kiasi kidogo,” kilieleza chanzo cha NIPASHE Jumapili kutoka moja ya taasisi zinahusika katika ziara hiyo.
MASANJA NA SHILOLE WAELEKEA WASHINGTON,DC KWENYE SHEREHE YA MIAKA 3 YA VIJIMAMBO NA TAMASHA LA UTAMADUNI WA KISWAHILI.
Wasanii Masanja Mkandamizaji na Shilole wakikwea pipa kuelekea Washington, DC kwenye sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo na Tamasha la Utamaduni wa Kiswahili Marekani litakalofanyika July 6, 2013 kuanzia saa 4 asubuhi (10:00 am) na Rais Mustaafu Ali Hassan Mwinyi ndiye atakayekua mgeni wa rasmi. Mhe. Ali Hassan Mwinyi anatarajiwa kufika Washington, DC siku ya Alhamisi July 4, 2013.
PICHA KWA HISANI YA Mo blog
RAIS KIKWETE AWAANDALIA MARAIS DHIFA YA KITAIFA YA CHAKULA CHA USIKU
Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Mfalme wa Swaziland, King Mswati katika hafla ya chakula cha usiku alichokiandaa kwenye viwanja vya Gymkhana, Dar es Salaam jana usiku, kwa waliohudhuria Mdahalo wa Kimataifa wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia kwa Manufaa ya Wote (Global Smart Partinership Dialogue). TBL ni moja kati kampuni zilizofadhli hafla hiyo.
Mahali palipoandaliwa kwa dina kwenye viwanja vya Gymkhana
Rais wa zamani wa Msumbiji, Joachim Chisano (kushoto) akikaribishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernald Membe katika hafla ya chakula cha usiku.
JK akiwa na Museveni wa Uganda (kushoto), Kingi Mswati wa Swaziland na Mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi
Saturday 29 June 2013
ZIARA YA OBAMA AFRIKA YA KUSINI KATIKA PICHA
Rais Obama kushoto na Michelle kulia wakikaribishwa na Jacob Zuma na mkewe Tobeka latika jumba la Umoja,Pretoria
Rais Barack Obama na mkewe Michelle Obama,kushoto, akipunga.Wa pili kulia ni rais wa Afrika ya kusini Jacob Zuma, na mkewe Tobeka Madiba Zuma, kulia, katika ngazi za jengo la Umoja lililopo Pretoria, Afrika ya kusini,Jumamosi juni 29.
WAZIRI MKUU MHE. MIZENGO PINDA NA MATUKIO BAADA YA KUAHIRISHA BUNGE MJINI DODOMA
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Spika wa Bunge, Anne Makinda baada ya kuashirishwa kwa kikao cha Bunge Mjini Dodoma Juni 28, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)Spika wa Bunge Mama Anne Makinda akizungumza na mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni 28,2013. (Picha na Ofisi ya Wairi Mkuu)Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Mkewe Tunu wakizungumza na Spika wa Bunge Mama Anne Makinda (katikati) kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni 28,2013. (Picha na Ofisi ya Wairi Mkuu)Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipongezwa na mkewe Tunu kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni 28,2013 baada ya hotuba yake ya kuahirisha kikao cha Bunge Mjini Dodoma . (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
NMB YAENDELEA KUZINDUA BUSINESS CLUB “SASA NI ZAMU YA KARATU”
Mhandisi mkuu wa Wilaya ya Karatu, Tulinumpoki Mwakalukwa akitoa shukrani zake kwa NMB mara baada ya kuzindua rasmi NMB Business Club wilaya ya Karatu. Kushoto ni Meneja wa NMB tawi la Karatu , Evarist Mtaro na mkuu wa kitengo cha wajasiliamali wadogo wadogo na wakati wa NMB Filbert Mponzi.
………………………………………………………..
Benki ya NMB imeendelea kuwa kinara katika kubuni na kuboresha huduma mbali mbali za kibenki, ili kuwawezesha wateja wake kupata unafuu na urahisi wa upatikanaji wa huduma za kibenki nchini Tanzania.
Katika kulizingatia hili, NMB imezidi kuzindua klabu maalum za wafanyabiashara maarufu kama NMB Business Club. Hadi sasa zaidi ya NMB Business Club 29 zimekwisha zinduliwa nchi nzima.
Kupitia NMB Business Club wajasiliamali wanaowezeshwa na benki ya NMB wamekua wakipata nafasi ya kujifunza jinsi ya kuandika michanganuo ya biashara zao na pia kuendelea kua vinara wa biashara.
Mkuu wa kitengo cha wajasiliamali wadogo wadogo na wakati wa NMB ,Filbert Mponzi akimkabidhi mwenyekiti wa NMB Business Club Paulith Jack mara tu baada ya kuibuka kidedea kwenye mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa NMB Business Club Karatu .
Sehemu ya wanachama wa NMB Business Club wilaya ya Karatu wakifurahia uzinduzi wa NMB Business Club.
CHANZO:Full shangwe
Subscribe to:
Posts (Atom)
PALM TREES ARE BEAUTIFUL
Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...
-
Dar es Salaam: Mwekezaji Sheikh Salim Abdullah ametangaza kuwekeza kwenye Uwanja Wa Ndege wa Kimataifa wa JK Nyerere Dar es Salaam (JN...