Friday 10 January 2014

Kashfa ya mapenzi yamwandama Hollande


Kashfa hii imetokea wakati Hollande akikabiliwa na kipindi kigumu cha utawala wake

Rais wa Ufaransa François Hollande, ametishia kuwachukulia hatua za kisheria wahariri wa jarida moja nchini humo lililochapisha taarifa za uvumi kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na mwanamke mmoja muigizaji JulieGayet.
Hollande hakukanusha madai hayo lakini alisema kuwa jarida hilo limekwenda kinyume na maadili ya vyombo vya habari kwa kuingilia maisha yake binafsi.

Bi Gayet mwenye umri wa miaka 41 ni muigizaji msifika wa vipindi vya televisheni.Jarida hilo, Closer,limechapisha picha kadhaa ambazo linasema zinathibitisha madai kuwa Hollande ana uhusiano wa karibu sana na Bi Gayet.

Duru zinasema kuwa ufichuzi huu umetokea wakati ambapo Hollande anakabiliwa na changamoto kadhaa katika utawala wake, ikiwemo kudorora kwa uchumi jambo ambalo wananchi wanamtarajia kulishuhughulikia.
Inajulikana wazi kuwa bwana Hollande ana mpenzi mmoja tu ambaye ni mwanahabari Valérie Trierweiler.
Hollande pia aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanasiasa mwenzake wa chama cha kisosholidti, Ségolène Royal.
Mwezi Machi mwaka jana aliwasilisha malalamiko yake kwa kiongozi wa mashitaka Jijini Paris, dhidi ya wanablogu na wenye Mitandao ya kijamii kuwa wanaeneza uvumi.
CHANZO: BBC

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...