Kamshna Msaidizi Kitengo cha Walemavu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Beatrice Fungamo (kulia), akimkabidhi Mwakilishi wa Mahabusu ya Watoto Upanga, Regina Kuname msaada wa vyakula na kitoweo cha mbuzi na mafuta ya kula kwa ajili ya kusherehekea Sikukuu ya ya Idd El Haji Dar es Salaam leo asubuhi.
Showing posts with label JAMII. Show all posts
Showing posts with label JAMII. Show all posts
Wednesday, 23 September 2015
COLLEGINE SISTERS OF HOLY FAMILY ORPHANAGE -TANGA
Tarehe 14/9 nilitoa mada kuhusu kituo cha kulea watoto
wasiokuwa na wazazi kiitwacho collegine sisters of Holf Family Orphanage
kilichopo Tanga,Tanzania.Wengi waliniandikia baada ya kuguswa na watoto hawa na
walitaka na wao kuchangia. Ifuatayo ni
namba ya sister ambae mnaweza kuwasiliana nae.Sister anaitwa Marcelina na namba
yake ni 0765 565 007.
KUTOA NI MOYO NA SI UTAJIRI.TUWASAIDIE
WATOTO HAWA KWANI WANAHITAJI MISAADA YETU KWA DHATI.

Sophia, mtoto mwenye umri wa miezi 5, ni mmoja kati ya watoto 54 wanaolelewa kituoni hapo
Unaweza kuingia katika website yao hapa vilevile uone njia nyingine za kuchangia
https://suorecolleginetanga.wordpress.com
Monday, 21 September 2015
PICHA NJE YA MAHAKAMA BAADA YA MWIMBAJI WA GOSPEL EMMANUEL MBASHA KUSHINDA KESI YA KUBAKA
Emmanuel Mbasha akiwa amepiga magoti huku akitokwa machozi nje ya Mahakama ya Ilala, Dar es Salaam baada ya Hukumu kutolewa.
Monday, 14 September 2015
TUSAIDIE WATOTO HAWA: COLLEGINE SISTERS OF HOLY FAMILY ORPHANAGE
Nilipokuwa jijini Tanga hivi karibuni nilibahatika kutembelea
kituo cha watoto kijulikanacho kama COLLEGINE SISTERS OF HOLY FAMILY ORPHANAGE (Nyumba
ya furaha).Kituo hiki kipo karibu na ilipokuwa Plaza Inn.Katika safari hii
ambayo ilikuwa ni ya kifamilia tuliambatana mimi na ndugu zangu.
Kabla ya kwenda kituoni hapo,tuliwasiliana na masista walezi
wa kituo hicho ili kujua mahitaji halisi kwa watoto hao kwani tulidhani ni
vizuri kufanya hivyo kuliko kupeleka tu vitu hata visivyo na ulazima.
Hii tulifanya vizuri sana kwani tuliweza kugundua kuwa kuna
watoto wachanga kabisa ambao walikuwa na mahitaji zaidi.
Siku moja kabla ya kwenda kituoni hapo tulinunua mahitaji kama
walivyotaka.Siku hii kulikuwa na mvua kubwa ila haikutuzuia kufanya manunuzi.
Tulinunua maziwa, lactogen 1 & 2, pampers na juice. Hivi ndiyo vitu
walivyotaka tuwapelekee.
Mtoto mdogo kuliko wote, Sophia, miezi mitano (5).Aliokotwa akiwa na siku 3 baada ya kuzaliwa

Mtoto George mwenye umri wa miezi 7
Bonyeza READ MORE kusoma habari yote na kuona picha zaidi
COLLEGINE SISTERS OF HOLY FAMILY ORPHANAGE
Nitaleta stori ya kituo hiki na nitaomba kuungwa mkono na wale wote wenye mapenzi mema.Bado ninaiandaa.Endelea kufuatilia hapa.
Saturday, 4 April 2015
DR. REGINALD MENGI NA JACQUELINE NTUYABALIWE WAFUNGA NDOA
Just Married: Bwana na Bibi Reginald Mengi
Ilikuwa ni furaha, upendo wa dhati na shangwe pomoni.
Baada ya miaka kadhaa ya uhusiano thabiti na uliokuwa umetawaliwa na upendo usio kifani, Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Limited, Dr. Reginald Mengi na Miss Tanzania, 2000, Jacqueline Ntuyabaliwe wamefunga ndoa.

Mimi Dr. Reginald Mengi naahidi kumpenda Jacqueline Ntuyabaliwe katika shida na raha hadi kifo kitutenganishe
Wawili hao wamebahatika kupata watoto wawili mapacha pamoja. Watoto hao wa kiume nao waliungana na wazazi wao kushuhudia wazazi wao wakibadilisha viapo vya ndoa.
Ilikuwa ni furaha, upendo wa dhati na shangwe pomoni.
Baada ya miaka kadhaa ya uhusiano thabiti na uliokuwa umetawaliwa na upendo usio kifani, Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Limited, Dr. Reginald Mengi na Miss Tanzania, 2000, Jacqueline Ntuyabaliwe wamefunga ndoa.
Mimi Dr. Reginald Mengi naahidi kumpenda Jacqueline Ntuyabaliwe katika shida na raha hadi kifo kitutenganishe
Wawili hao wamebahatika kupata watoto wawili mapacha pamoja. Watoto hao wa kiume nao waliungana na wazazi wao kushuhudia wazazi wao wakibadilisha viapo vya ndoa.
Tuesday, 31 March 2015
FILAMU INAYOANGAZIA MASAIBU YA ALBINO
Katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na ongezeko kubwa la mauaji ya albino, hasa katika mataifa ya Malawi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Tanzania na vile vile Burundi.
Watu hao hulengwa kutokana na itikadi za kichawi kwa madai kuwa viungo vyao huleta utajiri, bahati na kuponyesha maradhi yoyote.
Filamu moja inayoangazia mauaji ya albino Tanzania imezinduliwa London wiki hii,
Zuhura Yunus wa BBC alihudhuria uzinduzi huo.
CHANZO: BBC
Sunday, 8 June 2014
MSICHANA ANG’ATWA NA KUCHOMWA NA PASI NA MWAJIRI WAKE
Hali
ya msichana Yusta Lucas mwenye umri wa miaka 20
aliyefanyiwa ukatili wa
kufungiwa ndani kwa zaidi ya mwaka mmoja
huku akipewa adhabu ya kunga'twa na kuchomwa kwa pasi na mwajiri wake Amina Maige wa Mwananyamala jijini
Dar es salaam inaendelea vizuri kufuatia
matibabu anayopata ya majeraha yaliyomsababisha kupoteza fahamu.
Tuesday, 3 June 2014
Thursday, 22 May 2014
JE, UNA NINI LA KUSEMA JUU YA UKATILI USIOKUWA WA KAWAIDA KWA MTOTO ULIOTOKEA MJINI MOROGORO
Tuesday, 22 April 2014
MISS TANZANIA WAWILI WAJITANGAZA KUWA NA TATIZO LA ‘ENDOMETRIOSIS’ LINALOSABABISHA UGUMBA ILI KUWAPA MOYO WANAWAKE WENGINE
Miss Tanzania wawili, Happiness Millen Magese (2001) na Angela Damas (2002), wamejitokeza na kujitangaza wazi kuwa ni miongoni mwa mamilioni ya wanawake duniani wanaosumbuliwa na tatizo liitwalo ‘endometriosis’ ambalo huwafanya wapate maumivu makali wakati wa hedhi na pia kuwafanya wasiwe na uwezo wa kushika mimba.

Tuesday, 4 March 2014
UJAJI WA MABASI YAENDAYO KASI UTAPUNGUZA ADHA HII?

Usafiri wa daladala jijini Dar ni moja ya usafiri wenye mikikimikiki mingi kutokana na abiria kuwa wengi kupita uwezo wa basi hivyo kupelekea abiria kugombea nafasi.Kama hii haitoshi abiria wengi husimama ndani ya mabasi hivyo kuleta hali ya mashaka kwa abiria kwani wezi nao hutumia mwanya huo kuwaibia abiria.Abiria wengi hukumbwa na janga hili kila siku.Hapa ndiyo linakuja swali je, mabasi yaendaho kasi yaramaliza hili tatizo?
PICHA: James Nindi
Friday, 28 February 2014
TUKUMBUKE KURUDISHA KWA JAMII:KUTANA NA MDAU JAMES NINDI
| PICHA: Mdau James Nindi akiwa na watoto wanaoishi katika mazingira magumu leo jijini Dar,James ambaye mbali na kuwa na taaluma ya uandishi wa habari vilevile yeye ni social worker.Ameiomba jamii kuwa na utaratibu wa kuwatembelea watoto hawa na kuwasaidia pale tunapoweza,Anaamini kuwa pamoja inawezekana. HONGERA SANA JAMES! |
Friday, 24 January 2014
EXCLUSIVE INTERVIEW: PENNY AZUNGUMZA UKWELI WA MAMBO, ASEMA YEYE NA DIAMOND WAMEPEANA ’SPACE’ (VIDEO)
Mtangazaji na meneja wa vipindi wa kituo cha runinga cha DTV, Penniel Mwingila aka VJ Penny, amesema kuwa yeye na mpenzi wake, staa wa ‘My Number One’, Diamond Platnumz, wamepeana nafasi ili kila mmoja kutafakari anachotaka maishani.

Kauli ya Penny kwenye mahojiano maalum na Bongo5 TV, inajibu maswali ya wengi kuhusiana na kama wawili hao wapo pamoja au wameachana baada ya Diamond na mpenzi wake wa zamani, Wema Sepetu kurudiana tena. Katika interview hiyo, Penny ameongea pia kuanzia historia yake, namna alivyoingia kwenye utangazaji, alivyokutana na Diamond, mapenzi yao yalivyokuwa, alivyojisikia baada ya kuona picha za Wema na Diamond, maisha yake ya sasa na mipango yake ya mwaka huu.
Kauli ya Penny kwenye mahojiano maalum na Bongo5 TV, inajibu maswali ya wengi kuhusiana na kama wawili hao wapo pamoja au wameachana baada ya Diamond na mpenzi wake wa zamani, Wema Sepetu kurudiana tena. Katika interview hiyo, Penny ameongea pia kuanzia historia yake, namna alivyoingia kwenye utangazaji, alivyokutana na Diamond, mapenzi yao yalivyokuwa, alivyojisikia baada ya kuona picha za Wema na Diamond, maisha yake ya sasa na mipango yake ya mwaka huu.
Tuesday, 21 January 2014
JE,NI SAHIHI KWA GARI AINA YA TOYOTA NOAH KUBEBA ABIRIA?
Wadau,swala la ajali limezidi kuwa tatizo kubwa nchini kwetu kwani kila kukicha ni lazima tutasikia kuna ajali ya gari imetokea mahali.Hivi nini ni chanzo cha ajali hizi zisizokwisha? Je,ni kweli kwamba tumeshindwa kabisa kutatua tatizo hili? Maisha ya watu yataangamia mpaka lini?Hivi tuna watu wangapi ambao wamepata ulemavu wa kudumu kutokana na ajali hizi? Je,ni watoto wangapi wamebaki yatima kutokana na ajali hizi?Binafsi nashindwa kuelewa kuwa tatizo ni kutokuwa na madereva wenye kiwango kinachotakiwa au magari mabovu,ama vyote kwa pamoja.
Kitu kilichonishangaza zaidi ni kuona kuwa gari hizi ndogo aina ya Toyota Noah kutumika kama gari za abiria!Ni nani ametoa kibali katika biashara hii?Alifikiria mbali au aliangalia nini?Kwa mtazamo wangu gari hii inatakiwa kutumika kwa matumizi ya kawaida ndani ya mji na si kufanya safari za masafa marefu na abiria.Kwa mara ya kwanza niliambiwa gari hizi zinabeba abiria kati ya Tanga na Korogwe nikashangaa na kutokuamini.Nilipoona taarifa ya ajali mbaya ya Singida ndipo nikakumbuka.Watu wasiokuwa na hatia wamepoteza maisha kwa tatizo ambalo lineweza kuzuiwa.Mungu azilaze roho za marehemu wote wa ajali ya Singida mahali pema peponi,amen.
Wadau,tujadili nini kifanyike ili kupunguza tatizo hili.Unaweza kutuma maoni yako na tutayatoa hapa.Nakaribisha mjadala ili tunusuru maisha yetu!
Noah ilivyo nje
Noah ilivyo ndani
SOMA ALICHOANDIKA DIAMOND PLATNUMZ KWENYE INSTAGRAM
diamondplatnumz: Kama unakumbukumbu nzuri wakati nafanya tamasha langu la Christmass na Ngololo niliuliza mtoto atakae cheza vizuri Ngololo na kushinda nimpe zawadi gani?...na wengi walisema Nimuendeleze kielimu.... Hawa ndio washindi wetu walioshinda siku ile, ambao siku ya leo niliwapeleka Rasmi katika Shule ya East Africa International School
iliyopo Mikocheni Dar es salaam ili waanze Masomo yao...Niliona ni vyema kama mtoto yupo shule ya kawaida nimuhamishe international school ili niweze kumsaidia elimu bora zaidi...Niushkuru pia uongozi Mzima na wanafunzi wa Shule ya East Africa International School kwa kuwapokea vizuri
KWA PICHA ZAIDI BOFYA "READ MORE"
Friday, 10 January 2014
LULU AMSHANGAZA MAMA KANUMBA
Stori: Hamida Hassan na Imelda Mtema
MSANII wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’, mwanzoni mwa wiki hii alimshangaza (surprise) mama wa mpenzi wake wa zamani, marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa wakati alipokuwa akisherehekea miaka 58 tokea alipozaliwa.
MSANII wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’, mwanzoni mwa wiki hii alimshangaza (surprise) mama wa mpenzi wake wa zamani, marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa wakati alipokuwa akisherehekea miaka 58 tokea alipozaliwa.
Kumshangaza huko kumekuja baada ya Lulu kufika nyumbani kwa mama Kanumba, Kimara Temboni jijini Dar akiwa na bonge la keki, jambo ambalo mama huyo hakulitarajia.
“Yaani mama Kanumba alikuwa hajui kuwa Lulu anajua siku yake ya kuzaliwa, Lulu akatumia nafasi hiyo kumfanyia ‘sapraizi’,” alisema rafiki wa karibu wa Lulu aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Wednesday, 8 January 2014
HAKUNA HALI YA UMASKINI INAYODUMU MILELE-SOMA KISA HICHI CHA KUTIA MOYO HAPA

Kijana asiye na kazi aitwaye Nolesy aliamua kumwoa rafiki yake wa muda mrefu aliyekuwa akifanya kazi katika benki moja mashuhuri.
Nolesy alijitosa katika ndoa licha ya hofu na ushauri mwingi aliopewa na ndugu kuwa ni vibaya kuoa ukiwa huna kazi.
Kila mwezi yule binti alimpa mmewe mshahara wake
wote wa 800,000 baada ya kutoa fungu la kumi kwa ajili ya kanisani.
Nolesy alijitosa katika ndoa licha ya hofu na ushauri mwingi aliopewa na ndugu kuwa ni vibaya kuoa ukiwa huna kazi.
Kila mwezi yule binti alimpa mmewe mshahara wake
Monday, 30 December 2013
DUNIANI KUNA MAMBO: SHABIKI WA CHELSEA ALIYEISHI KWENYE HANDAKI MIAKA MINNE JIJINI DAR
• Yanga, Simba zamvutia lakini ashindwa kuchagua aipende ipi
• Asisitiza kama vipi, bora ziwe zinatoka sare kila mechi
• Asisitiza kama vipi, bora ziwe zinatoka sare kila mechi
UNIA ina maajabu yake ndiyo maana wakasema, “tembea uone”. Katikati ya Jiji la Dar es Salaam, binadamu ameamua kuishi ndani ya handaki kwa miaka minne.
Wednesday, 25 December 2013
RAIS KIKWETE ATOA ZAWADI YA KRISMASI
Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Beatrice Fungamo (katikati) akimkabidhi Mwakilishi wa Makao ya Watoto Kurasini wilayani Temeke Bibi Beatrice Mgumiro mbuzi tatu(3), kilo 150 za mchele na lita ishirini za mafuta ya kupikia ikiwa ni zawadi ya Krismas zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete. Zawadi hizo ambazo ni mbuzi, mchele na mafuta zilitolewa na Rais Kikwete ili kuwakumbuka watoto walio katika makundi maalum ili nao washerekehe sikukuu.
Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Beatrice Fungamo (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Kituo cha Mahabusu ya Watoto Ramadhani Yahaya (kulia) mbuzi mbili (2), kilo 100 za mchele na lita ishirini za mafuta ya kupikia ikiwa zawadi ya Krismas zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete. Zawadi hizo ambazo ni mbuzi, mchele na mafuta zilitolewa na Rais Kikwete ili kuwakumbuka watoto walio katika makundi maalum ili nao washerekehe sikukuu.
Subscribe to:
Posts (Atom)
PALM TREES ARE BEAUTIFUL
Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...
-
Hip Hop’s Legend, Jay Z announced his world tour yesterday which includes seven stops in Africa, according to Billboard. Jay-Z has nai...
-
Dar es Salaam: Mwekezaji Sheikh Salim Abdullah ametangaza kuwekeza kwenye Uwanja Wa Ndege wa Kimataifa wa JK Nyerere Dar es Salaam (JN...
-
Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...