Tuesday, 3 June 2014

KIFO CHA MTOTO NASRA MAARUFU KAMA "MTOTO WA BOKSI" KIWE CHACHU YA KUKOMESHA UKATILI KWA WATOTO

Mtoto Nasra,enzi ya uhai wake.

Mtuhumiwa no.1:Rashid Mvungi,baba       Mtuhumiwa no.2: Mariam Said,
wa Nasra                                                   mama mlezi


Mtuhumiwa wa tatu, Mtonga Omar, baba mlezi wa Nasra


Kutokana na kifo cha kusikitisha cha motto Nasra naomba tujadiliane.
Hivi hawa waliomfanyia ukatili mtoto Nasra Mvungi,”maarufu kama mtoto wa boksi ”wapewe adhabu gani?Tukumbuke mwanzo walishatakiwa kwa kutuhumiwa kumfanyia mtoto Nasra ukatili. Kwasasa mtoto Nasra amefariki kutokana na madhara aliyoyapata kutokana na ukatili wa kupitiliza  aliofanyiwa. Kwanza, natumaini mashtaka yao yatabadilishwa na kuwa mauaji.Je, wewe mdau unayesoma hapa,ungefarijika kama watu hawa wangepewa adhabu gani? Je,tunahitaji watu kama hawa kwenye jamii yetu?
Hapo ulipo,hakuna mtu / watu wanaofanyia watoto/ mtoto ukatili unaofanana na huu?Kama wapo,umefanyanini kusaidia?
Je, unataka kumuenzi vipi mtoto Nasra?

CHUKUA HATUA ILI KULINDA UHAI WA WATOTO.
Na Anna Nindi

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...