1.
PASTA
Hiki ni
chakula cha haraka.Unaweza kutayarisha pasta kwa kuongeza tu protini ulizonazo
katika jokofu lako mfano kuku,nyama ya kusaga, kamba(prawns) n.k.Ili kuzifanya
pasta zako ziwe tamu pasha ½ kikombe cha mafuta ya zeituni(olive oil) kikaangoni,weka
spinachi,nyanya au uyoga.Pika kwa dakika 3 au mpaka mboga zilainike. Ongeza
chumvi na pilipili(kama unatumia pilipili).Changanya pasta zako ambazo
zimepikwa tayari katika mchanganyiko huu wa mboga.
2. CHICKEN BROTH OR BOUILLON
Unaweza
kutengeneza mchuzi au supu kwa kutumia chicken broth pamoja na viungo vingine
ulivyonavyo jikoni kwako na kupata mlo mzuri kabisa. Mfano unaweza kuongeza
mbogamboga au nyama nk.Unaweza kutumia hii katika kuongeza ladha kwenye kuku wa
kuoka,kupikia wali na hata mbogamboga badala ya kutumia maji.
3.
MBOGA
ZILIZOGANDISHWA/ZILIZOHIFADHIWA KATIKA KOPO
Unaweza kuzipasha kwa kuchanganya
na chicken broth ukapata mchuzi au supu.Unaweza kuongeza ladha kwa kutupia
vipande vya kuku na viungo vingine utakavyo kuweka ladha.
4.
KUKU
Unaweza
kupika kuku katika njia nyingi tofauti.Unaweza kuchanganya na mbogamboga,
kumchoma/kuoka, kukaanga n.k.Mimi binafsi kuku na samaki zinakamilisha kabisa
mlo wangu na huwa havikosekani jikoni kwangu.Kuku nzuri kuwa nayo ni ambayo
ambayo imetolewa mifupa.
5.
VIAZI
Viazi
kama ilivyo kwa kuku,huweza kutumika kutayarisha idadi kubwa ya chakula.Viazi
huweza kutumika katika supu au mchuzi.Vilevile vinaweza kuokwa, kuchemshwa,
kukaangwa katika aina nyingi tofauti.
6.
MAYAI
Hiki ni kiungo kikubwa na muhimu sana
jikoni.Mayai hayatumiki kwa kifungua kinywa tu, huweza vilevile kutumika
kutengeneza vyakula kamili.
7.
NYAMA YA
KUSAGA
Hiki ni kiungo muhimu kwani unaweza kutengeneza vyakula
tofauti kwa kutumia nyama ya kusaga mfano mkate wa nyama,meat balls, tacos,
hamburgers n.k.Unaweza kuongeza ladha kwa kuongeza kitunguu thoum, pilipili
manga/pilipili ya unga,chumvi n.k
8.
MCHELE
Mchele
unaweza kutumika kutengeneza mlo kamili mfano risotto, sushi, supu ya kuku na mchele,
jambalaya au pilau. Aina tofauti za mchele
zijulikanazo ni arborio, jasmine, basmati n.k
9.
NYANYA YA KOPO/BOKSI
:Nyanya ni kiungo muhimu katika mchuzi au supu. Unaweza
kuchanganya nyanya na viungo tofauti na kutengeneza sosi yako mwenyewe kwaajili
ya pizza au pasta.
10.
BACON
Unaweza
kutupia bacon katika pasta, viazi au supu na kuongeza ladha katika mlo wako.
No comments:
Post a Comment