HERUFI A
Mwenye jina linaloanziana na herufi A ni mtu anayependa mambo makubwa,
anajiamini na mwenye uwezo wa kutimiza malengo yake. Ni mtu mwenye tahadhari, mchangamfu na mpenda
matukio. Anapenda Kuheshimiwa, anapenda Mamlaka, na ana kiburi, na hasira.
HERUFI B
Mwenye jina linaloanziana na
herufi B ni mtu, mkarimu, muaminifu, na hupenda kazi. Ni Jasiri, shujaa na
mkatili katika vita au pale anapotaka kulinda vilivyo katika himaya yake.
HERUFI C
Mwenye jina linaloanziana na
herufi C ni mtu wa kukubadilika badilika, mshindani na hupenda kupigania
malengo yao wanayopenda. Ni watu wa wabunifu na wanaopenda mawasiliano.
HERUFI D
Mwenye jina linaloanziana na
herufi D ni mtu anayependa usawa, Biashara. Ni watu wanaopenda kuamrisha na
mwenye kupenda usafi. Ni jeuri na wenye msimamo.
HERUFI E
Mwenye jina linaloanzia na
herufi E ni mtu mwenye roho nzuri ,yenye mapenzi na huruma. mwenye kupenda
uhuru katika mapenzi na mchangamfu. Kinyume na hivyo atakuwa ni mtu
asiotegemewa na kigeugeu.
HERUFI F
Mwenye jina linaloanzia na
herufi F ni mtu mwenye mapenzi,huruma , roho nzuri na ana uwezo wa kuwafariji
watu. Ni mtetezi wa watu na mwenye huzuni lakini ni mzito wa kufanya maamuzi.
HERUFI G
Mwenye jina linaloanzia na
herufi G ni mtu mwenye mwenye imani ya kidini na nguvu za kiroho. Ana kipaji
cha kubuni na uwezo wa kutatua matatizo ya watu. ni mtu mwenye hisia
kali,msomi, mpweke na mkaidi wa kukubali ushauri wa kutoka kwa watu.
HERUFI H
Mwenye jina linaloanzia na
herufi H ni mtu mwenye ubunifu na nguvu katika biashara, hupata faida kubwa
kutokana na jitihada na bidii zake. ni mwenye mawazo mengi, mchoyo na mbinafsi.
HERUFI I
Mwenye jina linaloanzia na
herufi I ni mtu mwenye kupenda sheria, ana huruma na utu. Wakati mwingi
hajiamini na ni mwenye hasira za haraka.
HERUFI J
Mwenye jina linaloanzia na
herufi J ni mtu mwenye matamanio,mkweli, mkarimu na muerevu. asiyekubali
kushindwa na hupata mafanikio makubwa. Wakati mwingine anakuwa ni mtu mvivu na
aliyekosa mwelekeo.
HERUFI K
Mwenye jina linaloanzia na
herufi K ni mtu mwenye jeuri. mwenye msimamo thabiti,mashuhuri na mwenye uwezo
wa kushawishi na kuamsha hisia za watu wana uwezo wa utambuzi ambao watu wengi
hawana. ni mtu asioridhika na hali ya kimaisha.
HERUFI L
Mwenye jina linaloanzia na
herufi L ni mtu wa vitendo, mwenye hisani na aliyejipanga vizuri kimaisha. Huwa
wanapata ajali mara kwa mara.
HERUFI M
Mwenye jina linaloanzia na
herufi M ni mtu mwenye kujiamini sana, mchapakazi na hupata mafanikio. ni mtu
mropokaji,mwenye haraka na mwepesi kukasirika.
HERUFI N
Mwenye jina linaloanzia na
herufi N ni mtu mwenye ubunifu, hisia kali na hupenda kuwasiliana lakini ana
wivu sana.
HERUFI O
Mwenye jina linaloanzia na
herufi O ni mtu mwenye subra, mvumilivu na mwenye bidii ya kusoma. Ni mtu
mwenye kupenda kutumikia jamii na mwenye uwezo mkubwa wa kudhibiti hisia.
HERUFI P
Mwenye jina linaloanzia na
herufi P ni mtu mwenye uwezo wa kuamrisha na hekima kubwa. Ana nguvu za kiroho
lakini anapenda sana kujitumbukiza kwenye mambo ya watu.
HERUFI Q
Mwenye jina linaloanzia na
herufi Q ni mtu mwenye kupenda mambo ya asili. Ni watu wasiyoelezeka nawana
uwezo wa kuonyesha vitu visivyojulikana hata hivyo ni mtu aliyepooza sana.
HERUFI R
Mwenye jina linaloanzia na
herufi R ni mtu mwenye uvumilivu, wenye huruma lakini ana hasira za haraka.
Muda wote anakuwa mpenda amani.
HERUFI S
Mwenye jina linaloanzia na
herufi S ni mtu mwenye mvuto mkali wa kuleta utajiri. Ni watu wenye maamuzi ya
ghafla na hupenda mageuzi makubwa.
HERUFI T
Mwenye jina linaloanzia na
herufi T ni mtu mwenye kupenda ushauri wa kiroho, anatumia nguvu za ziada
kusaidia watu na hupata mafanikio baada ya muda mrefu. Ni watu wenye hisia kali
sana na ni wepesi kushawishika.
HERUFI U
Mwenye jina linaloanzia na
herufi U ni mtu mwenye bahati kubwa kwa ujumla. Anapenda uhuru katika mapenzi.
Lakini ni mtu mbinafsi, mwenye tamaa na aliyekosa maamuzi.
HERUFI V
Mwenye jina linaloanzia na
herufi V ni mtu Mchapakazi, wenye bidii na asie choka. Hata hivyo ni watu
wasiotabirika.
HERUFI W
Mwenye jina linaloanzia na
herufi W ni mtu muwazi, wachangamfuu kupita kiasi na mwenye uwezo wa kutambua
mtu mwema na mbaya. Ni watu wenye tamaa na hufanya mambo ya hatari.
HERUFI X
Mwenye jina linaloanzia na
herufi X ni mtu asiyependa kuwekewa vizuizi katika kwenye anasa na ni rahisi
kujiingiza kwenye uzinzi na kujitoa uaminifu.
HERUFI Y
Mwenye jina linaloanzia na herufi Y ni mtu mwenye kupenda Uhuru na
hawapendi kupingwa jambo lao lolote. Ni watu wanaokosa uamuzi na husababishia
kupoteza bahati katika maisha.
HERUFI Z
Mwenye jina linaloanzia na herufi Z ni mtu mwenye kupenda matumaini na
amani. Ni wenye msimamo mkali ila wanashauriwa kufikiria kabla ya kuamua jambo,
Je na jina lako lina maana?
CHANZO: KAJUNASON BLOG
No comments:
Post a Comment