Monday 6 April 2015

TEMBEA UONE: ADHA YA SIMBA TUNDURU



Nikiwa Tunduru nilishtushwa sana na hadithi za simba waliokuwa wakijitokeza mara kwa mara mjini Tunduru. Hii siyo hadithi, ni matukio ya kweli.
Kipindi nilichokuwepo Tunduru ilikuwa ni mwezi wa Desemba na tukakuta stori kuwa mwezi wa septemba,simba aliingia mjini!Mdau, ingekuwa ni wewe katika mazingira haya ungejisikiaje? 


Yaani unapewa habari hizi siku ya kwanza tu kufika sehemu ambayo utakaa mwezi mzima!Kwa kweli taarifa hii ilininyima raha kabisa maana wakati mwingine tulikuwa tunamaliza kazi zetu usiku.Sehemu tuliyokuwa tunakaa ilikuwa karibu sana na eneo letu la kazi ila ilitubidi tuwe na usafiri tukitoka usiku. Palikuwa na msikiti jirani na msikiti huo ulisaidia sana kutoa matangazo mbalimbali wakati wa swala mchana au usiku, hususan kuhusu watoto waliopotea au kama simba kaonekana mjini.
Sijui kwasasa hali hiyo ya simba kuvamia makazi ya watu imekwisha au bado ni hivyo hivyo?
KWA KWELI TEMBEA UONE!

Imeandikwa na Anna Nindi

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...