Friday 3 April 2015

TEMBEA UONE: BIASHARA YA NDIZI TURIANI


Nilitembelea Turiani iliyopo katika wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro.Turiani kunasifika kwa kilimo cha miwa na ndiyo kuna kiwanda cha sukari cha Mtibwa.Wakazi wa Turiani ni wakulima. Asubuhi moja tukielekea katika shughuli iliyotupeleka pale,tukakutana na kijana anauza ndizi mbivu katika sinia kubwa alilobeba kichwani. Ndizi zilikuwa nzuri sana kwa kweli. Nilimuuliza bei ya ndizi. Bei aliyotutajia Yule kijana mimi na mwenzangu tukatazamana na kushangaa. 



Alipoona tumeshangaa kijana Yule akasema, “mshishtuke na bei,mnaweza kuomba heri”. Tukamuuliza kivipi? Akatujibu “Naona mmeshtuka nauza ghali,naweza kuwapunguzia bei.
Kilichotushtusha ni bei aliyotaja ilivyokuwa ndogo nab ado muuzaji alikuwa tayari kupunguza bei!
Tukagundua neno “kuomba heri” lilimaanisha “kupunguziwa bei”.Tulisikitika kuwa kijana Yule alikuwa anazunguka na sinia la ndizi ambalo kipato chake wala kisingekidhi mahitaji yake nabado alikuwa tayari kutupunguzia bei.
Tulimwambia tutatununua tu kwa bei anayouza bila ya kuomba heri.Tulinunua ndizi zake zote na kupelekea wenyeji wetu wale kila mtu kwa uwezo wake.

KWELI TEMBEA UONE!

Imeandikwa na Anna Nindi

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...