Nimegundua kuwa ni mama pekee ndiye mwenye mapenzi ya kweli
kwa mwanae. Mama yako hawezi kukutupa au kukukataa katika namna yeyote labda
awe na matatizo ya akili.
Mume au mke anaweza kukugeuka haijalishi mmetoka nae
wapi.Kweli sisi binadamu tunasahau haraka mno.Na kitu kibaya tunasahau hata
mema ambayo wenzi wetu wametutendea.Mtu anaweza kuamua kumfukuza mwenzi wake
kama mbwa na kusahau kabisa uzuri wa hayo maisha anayoishi kwasasa yamechangiwa
kiasi kikubwa na huyo anayemfukuza.Watu huacha mazuri yote waliyokuwa nayo
kabla ya kukutana na wenza wao na kuamua kuwafuata wenzao hao kutokana na
mapenzi.Watu huacha kazi zao nzuri na maisha mazuri waliyokuwa nayo kwaajili ya
mapenzi.Watu huuza na kuweka rehani vitu vyao vya thamani kwaajili ya mapenzi.
Watu hupoteza wapendwa wao wakati wakilinda penzi ILA mwishoni huyo
unayemfanyia hivyo hakumbuki yote haya.Anaacha mbachao kwa msala upitao.
Anapokuwa amepata mwingine hujali kukidhi tamaa zake za mwili,
basi.Kama ulimsadia hiyo ilikuwa ni charity tu kwake.Kuna watu wamezoea kuoa na
kuacha au kuolewa na kuachwa.Kwao haya ndiyo maisha,Na watu hawa ukiangalia
zaidi ya kuwa na nguo za kuvaa hawana asset yoyote. Watapata wapi asset wakati
wako busy na kutafuta wanawake/wanaume wapya kila siku ili kukidhi tu tamaa za
mwili?Mtu anazeeka hana chochote na bado ana matumaini kuwa ETI bado ana muda
wa kupata mali au kutengeneza maisha yake.Hapa ndipo unapoona maana ya ile
methali ``AKILI NI NYWELE KILA MTU ANA ZAKE``.
Mpaka unaweza kujiuliza hivi mtu huyu karogwa au ndiyo akili
yake?Kwanini mtu huna wivu wa maendeleo? Je, na wewe ni mmoja wao?
TAFAKARI NA CHUKUA HATUA.
No comments:
Post a Comment