Wengi hatujui haki zote na hii hupelekewa mtu kuonewa bila sababu. Soma hapa ujue haki zako uwapo mikononi kwa polisi.
( 1 )Askari akikuweka chini ya ulinzi
muulize kitambulisho ni haki yako.
( 2 )Askari akikukamata akuoneshe kitambulisho chenye muhuri wa
mahakama kama anasema ametumwa na mahakama kukumata, ni haki yako.
( 3 )Askari akikukamata akwambie kwanini
anakukamata na anakupeleka kituo gani, ni haki yako.
( 4 )Unaruhusiwa na sheria kukataa
kukamatwa hata kutumia nguvu kama hukuambiwa sababu ya
kukamatwa.
( 5 ) Askari anapokiuka taratibu za ukamataji
anageuka na kuwa mhalifu ni haki yako kujikinga naye.
( 6 )Askari haruhusiwi kukuvuta shati,
kukukaba koo, kukushika suruali kama hujakataa kutii amri halali.
( 7 )Askari haruhusiwi kuondoka na mtu
mwingine baada ya kumkosa mtuhumiwa halisi.
( 8 ) Askari haruhusiwi kupekua
nyumba ya mtu bila kibali cha kupekua.
( 9 )Askari lazima akuoneshe kibali cha kupekua
na ukisome.
( 10 )Kibali kieleze jina la aliyekitoa, kituo
kilipotolewa,jina la mtu au sehemu ya upekuzi, au uchanganuzi wa mtu au sehemu.
( 11 )Hairuhusiwi
kupekuliwa usiku kuanzia saa 1 jioni mpaka saa 12 asubuhi.
( 12 )Ni haki yako
kumpekua askari kabla hajakupekua ili asipandikize kitu.
( 13 )Usipekuliwa nyumbani
bila kuwapo kiongozi wa mtaa.
( 14 )Kila kitakachochukuliwa
katika upekuzi lazima kiandikwe na askari aweke sahihi.
( 15 ) Mali
iliyochukuliwa katika upekuzi lazima ibaki salama.
( 16 )Mwanaume haruhisiwi
kumpekua mwanamke na mwamke haruhisiwi kwa mwanaume.
( 17 )Unaruhusiwa kukataa kupekuliwa
iwapo taratibu hizi hazikufuatwa.
( 18 )Askari haruhusiwi
kukutukana wala kukupiga.
( 19 ) Unaruhusiwa
kutozungumza lolote mpaka unayemuamini afike uwapo chini ya ulinzi, ni haki
yako.
( 20 )Usilazimishwe kuongea au
kuandika ambacho hutaki, ni haki yako.
( 21 )Usitoe maelezo bila
uhakika yatatumika mahakamani yatakuletea shida.
( 22 )Unaruhusiwa kukaa kimya
na usizungumze kitu uwapo chini ya ulinzi.
HIZI ZOTE NI HAKI ZAKO,
ZILAZIMISHE USIBEMBELEZE WALA USIZIOMBE
CREDIT: sheriayakub bliog
No comments:
Post a Comment