Friday, 26 April 2013

NINI KIFANYIKE KUWAONDOA HAWA WATOTO MITAANI?


Jamii isaidie hawa watoto kwani kuwa kwao katika maisha haya ya mitaani kwa muda mrefu huwafanya wengi wasitake kurudi tena shule. Nakumbuka kuna rafiki yangu mmoja alimwona mtoto mmoja wa kiume akiwa anazunguka na kuomba kila siku.Rafiki yangu aliumia sana na kuona kuwa umri aliokuwa nao yule mtoto alistahili kuwapo shule.Alimuuliza yule mtoto kwanini haendi shule na badala yake anaomba barabarani?Mtoto alimwambia kuwa mzazi wake hakuwa na uwezo wa kumpeleka shule. Rafiki yangu akamuuliza mtoto kama alikuwa tayari kwenda shule endapo angelipiwa gharama zote na kupatiwa mahitaji yote ya shule. Mtoto alisema yupo tayari kurudi shule.
Rafiki yangu alimtafutia mtoto shule(msingi) ambayo angeweza kumfuatilia na alimwomba mwalimu wa darasa awe anampa ripoti ya maendeleo ya mtoto kwani aliwaeleza walimu historia ya mtoto. Alimnunulia mtoto yule sare za shule,madaftari,kalamu,soksi,viatu na begi la shule.
Mtoto alianza shule akiwa na sare mpya na begi lake mgongoni!Unajua ni nini kilitokea?Mtoto yule alikuwa akitoka shule anarudi ofisini kwake,yaani mtaani!Siku moja rafiki yangu akiwa mitaani akamwona yule mtoto ghafla akiwa anakimbilia watu na kuomba kama alivyowahi kumkuta awali kabla hajampeleka shule.Rafiki yangu aliumia sana kwani hakuwa na uhakika kama ndoto za kumsaidia mtoto yule zitafanikiwa.Akaenda akamshika mkono na kumwita jina lake na kumuuliza anafanyanini pale?Mtoto alishindwa kudanganya kwani alijua kuwa ameonekana akiomba.
Mtoto akamwambia rafiki yangu kuwa yeye maisha aliyozoea ni hayo ya mtaani hivyo swala la kurudi shule kwake ni gumu!Huo ndiyo ulikuwa mwisho wake kwenda shule.
Hii ilichangiwa sana na ukweli kwamba mtoto yule alishakaa mtaani muda mrefu na kuyazoea maisha yale.
Nadhani kabla ya shule alitakiwa apewe ushauri nasaha ili iwe rahisi  kwa akili yake kukubali kutoka hali moja ya maisha kwenda nyingine.
Kisa hiki si cha kutunga,ni cha kweli!

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...