Wamasai ni kabila la watu wahamaji wanaopatikana kaskazini mwa Tanzania. Kabila hili vilevile linapatikana nchini Kenya.
UTAMADUNI
Wamasai humwabudu Mungu mmoja pekee, na wao humwita Mungu Enkai au Engai. Engai ni Mungu mmoja mwenye asili mbili: Engai Narok ( Mungu Mweusi) ana huruma, na Engai Nanyokie (Mungu Mwekundu) ana ghadhabu.
Kipimo cha mali ya mtu ni idadi ya mifugo na watoto alionao
Wanawake wakimasa wakijenga nyumba
MAVAZI
Mavazi hutofautiana na umri, jinsia, na mahali. Vijana wa kiume, kwa mfano, huvaa nguo nyeusi kwa miezi kadhaa inayofuata tohara. Hata hivyo, nyekundu ni rangi inayopendelewa.
Wamasai huvaa makubadhi, ambayo hutengeneza kwa kutumia matairi ya magari au plastiki. Wanaume na wanawake kuvaa vikuku vya mbao.
Wamasai wanawake mara kwa mara hufuma marembesho na mikufu ya shanga. Ushanga huu huwa na sehemu muhimu katika urembesho wa miili yao. Ingawa kuna tofauti katika maana ya rangi ya shanga, baadhi ya maana kwa jumla ya rangi chache ni:
nyeupe- amani; bluu- maji; nyekundu- mpiganaji / damu / shujaa.
NYWELE
Kunyoa kichwa(kipara) ni kawaida katika sherehe za kubalehe(jando).Vilevile huwa ishara ya kutoka daraja moja kwenda jingine (huwakilisha mwanzo mpya kutoka sura moja ya maisha hadi nyingine). Morani ndilo kundi pekee katika jamii ya Wamasai wanaoruhusiwa kuwa na nywele ndefu, ambayo huifuma katika nyuzi ndogo ndogo.
Siku mbili kabla ya wavulana kutahiriwa, vichwa vyao hunyolewa. Morani hao huacha nywele zao zikue wakati huo wakitumia muda mwingi kusuka nywele zao. Hupaka nywele zao mafuta ya wanyama na udongo mwekundu(ocher). Pamba au nyuzi za sufu zinaweza kutumiwa kurefusha nywele. Nywele zilizosuka huachwa zikining´inia au hufungwa pamoja kwa ngozi. Morani wakiingia daraja la Eunoto , na kuwa wazee, nywele zao ndefu zilizosukwa hunyolewa.
Vilevile wanaume hunyoa nywele wanapopita daraja moja la maisha hadi jingine, Bibi arusi pia atanyolewa kichwa chake, na kondoo wawili dume huchinjwa kukamilisha sherehe hiyo.
Baadhi ya picha za wakina mama wa Kimasai
No comments:
Post a Comment