MSANII maarufu wa nyimbo za 'hip hop' na Bongo Fleva, Albert Mangwea maarufu kama Man Ngwair aka Ngwair ametangazwa kuwa amefariki dunia leo akiwa nchini Afrika Kusini katika hospitali ya St. Hellen ya jijini Johanesburg.
Kwa mujibu wa taarifa za redio mbalimbali jioni hii nchini, inadhaniwa huenda Ngwair amefariki dunia kutokana na matatizo ya matumizi ya dawa za kulevya.
Aidha, taarifa kutoka kwa mmoja wa mtu wa karibu wa Ngwair nchini humo, Hussein Original aliyepo mji wa Pretoria, alisema alikutwa amefariki wakati msanii mwenzake ‘M To The P’ alikutwa amepoteza fahamu majira ya asubuhi walipokwenda kuwagongea mlango gheto kwao. Daktari tayari alishathibitisha taarifa hizo na tayari ametoa taarifa kwa watu wa karibu wa msanii huyo. Akiongea na redio ya Clouds FM, mwenyeji mwingine wa Afrika Kusini aliyejitambulisha kwa jina la Jonathan amesema usiku wa kuamkia leo Mangwair alirudi nyumbani alikofikia akiwa mzima wa afya lakini mpaka kunakucha hakuonesha dalili za kuamka: “Sijui hata huko alitumia nini,” amesema Johnson. Amesema naye asubuhi kulipokucha aliondoka kuendela na mishemishe yake na alipokuwa huko wenzake walimpigia simu kumtaarifu kuwa wamempeleka Ngwair hospitali kwa kuwa alikuwa bado hajaamka.

Naye mwanamuziki Bushoke anayeishi jijini Pretoria amesema alikuwa akutane na Ngwair leo jijini Johannesburg lakini alishangaa kutompata kwenye simu. Amesema baada ya kuwatafuta washikaji ambao ni wenyeji wake ndipo walipomuambia kuwa Ngwair amefariki: “Unajua Ngwair ni mshkaji wangu sana yaani hata siamini kama amefariki aisee,” amesema Bushoke.
Bushoke amesema kesho amepanga kwenda Johannesburg kujionea mwenyewe.
Kimuziki, Ngwair aliibukia kwenye Dodoma ambako alikuwa katika kundi moja na Noorah na Mez B.
Baadaye akapata dili Bongo Records chini ya mmiliki wa studio hizo, Petter Matthysse ‘P Funk’ aliyemuinua zaidi kimuziki na kumfanya awe miongoni mwa wanamuziki nyota nchini.
Wimbo wake wa kwanza kutamba ni Gheto Langu mwaka 2003 ambao ulimpatia umaarufu kabla ya kutoa albamu yake ya kwanza a.k.a Mimi mwaka 2003 ambayo ilimpatia mafanikio makubwa na kubadili maisha yake.
Hata hivyo, mafanikio hayo yalimlevya na kujitumbukiza kwenye utumiaji wa dawa za kulevya, hivyo kujikuta akishindwa kufanya kazi ya muziki kwa usanifu na kuanza taratibu kufilisika hadi kuuza mali zake zote, ikiwemo gari aina ya Jeep.
Ngwair kutoka kwenye kupanga nyumba nzima maeneo ya Sinza, Dar es Salaam akajikuta anarejea kuishi katika ‘magheto’ ya washkaji zake sehemu mbalimbali Dar es Salaam.
Mwaka 2010, Athumani Tippo, mmiliki wa maduka ya Zizzou Fashions alijaribu kumuinua tena msanii huyo baada ya kumchukua kwenye lebo yake na kumuwezesha kutoa albamu ya pili, Nge.
Hata hivyo, Nge haikufanya vizuri sana na kuzidi kumchanganya msanii huyo hivyo kutopea kwenye dimbwi la utumiaji wa dawa za kulevya na ‘kuharibika zaidi’.
Mafanikio yake zaidi ni kushinda tuzo ya Kilimanjaro Music Awards kama mwana Hip Hop Bora wa mwaka 2005.
Mwaka 2003, msanii Wayne Wonder aliyekuja kutumbuiza kwenye Fiesta aliondoka na CD ya wimbo Mikasi ya Ngwair baada ya kuvutiwa na kibao hicho alichowashirikisha Mchizi Mox na Ferooz. Pumzika kwa amani. RIP Ngwair.
No comments:
Post a Comment