Friday 10 May 2013

DAVID MOYES KOCHA MPYA WA MANCHESTER UNITED


David Moyes (50) amesaini mkataba wa  miaka 6 kuinoa timu ya Manchester United. David anarithi mikoba wa kocha Alex Ferguson.Moyes anatokea timu ya Everton.
Ni heshima kubwa kuwa meneja wa timu ya  Manchester United,”alisema Moyes katika taarifa yake.

“Nina furaha kuwa Sir Alex  ameniona ninafaa na hivyo kunipendekeza mimi kwa kazi hii. Nina heshima kubwa kwa kila kitu ambacho  Sir Alex amekifanya na kwa timu.”

Jumatano iliyopita,Ferguson alitangaza kuwa anastaafu kazi ya umeneja nafasi ambayo amekuwa nayo kwa karibu miaka 27 Old Trafford.
Ferguson mwenye umri wa miaka 71 atabakia United kama Mkurugenzi.
CHANZO: Northjersey sports

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...