Faida za teknolojia
Inafanya maisha kuwa rahisi
Kwa kutumia mashine watu wanapata urahisi katika kila nyanja mfano gari na baiskeli humsaidia mtu kufika kule aendako haraka zaidi. Umbali kati ya nchi na miji umepunguzwa kwa kutumia ndege na treni za kasi.
Upatikanaji wa habari umerahisishwa kwa kutumia kumpyuta na intaneti. Kwa kutumia teknolojia ya mawasiliano(communication technology),watu wanaweza kufanya mikutano kwa kutumia video (video conference). Vilevile mtu anaweza kuwasiliana na ndugu na marafiki kwa kutuma ujumbe (chatting).
Hupunguza makosa ya kiutendaji
Utumiaji wa mashine husaidia watu kupunguza makosa katika kazi zao.Mfano,makampuni mengi ya uzalishaji hutumia mashine ambazo hufuata maelekezo kutoka katika kompyuta au mtu anayeiendesha mashine ile ili kufaanya kile kilichokusudiwa.Kazi hufanyika barabara.
Inaokoa muda
Teknolojia inaokoa muda mfano,unaweza kuruka kwa ndege kwenda sehemu yeyote kwa kutumia muda mdogo.Kwa kutumia kompyuta unaweza kufanya kazi yeyote kwa kutumia muda mdogo sana .
Mashine zanasaidia sana jikoni ambapo mpishi anaweza kuokoa sana muda.
Hasara za teknolojia
Kila kitu kizuri hakikosi mabaya yake.
Watu kupoteza kazi
Watu wengi wamepoteza kazi kutokana na kuwa makampuni mengi yanatumia mashine katika uzalishaji na shughuli nyingine za kiutendaji.
Gharama kubwa za mashine
Mashine nyingi huuzwa ghali.Vilevile matengenezo ya mashine zinapoharibika ni ghali.
Kutokana na sababu hizi si jambo rahisi kwa kila mtu kumudu kununua mashine mbalimbali kwa matumizi ya aidha nyumbani au kazini kwake.
Kwa leo ngoja tuangalie baadhi ya mashine mbalimbali ambazo huweza kutumika jikoni na kurahisisha kabisa utendaji na uokoaji wa muda
Mashine ya kumenya viazi |
Mashine ya kutengenezea kahawa (coffee maker) |
Sufuria la kupikia wali (rice cooker) |
Mashine ya kuchanganya na kusaga vyakula mbalimbali (blender) |
Mashine za kuoshea vyombo
Mashine ya kupashia moto chakula (microwave) |
Wadau,tumetaja mashine chache sana kati ya nyingi ambazo zipo.Tutaendelea kujuzana na kuelimishana kupitia rainbow-tz blog.
No comments:
Post a Comment