Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo ikulu jijini Dar es Salaam amemwapisha Jaji Aloycius Mujuluzi kuwa Mwenyekiti wa tume ya kurekebisha sheria pamoja na mabalozi wanne watakaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi.Mabalozi walioapishwa leo ni pamoja na Balozi mpya katika umoja wa Falme za kiarabu(UAE) Mbarouk Nassor Mbarouk,Balozi mpya wa Tanzania nchini Uholanzi Wilson Masilingi,Balozi mpya wa Tanzania katika visiwa vya Commoro Chabaka Kilumanga na Mwakilishi wa kudumu Tanzania Umoja wa mataifa Geneva Balozi Modest Jonathan Mero.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal na Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe wakiwa katika picha ya pamoja na mabalozi wapya waliopaishwa leo ikulu jijini Dar es Salaam.aliyesimama mbele kushoto no Balozi Liberata Mulamula anayekuwa Balozi Mpya wa Tanzania nchini Marekani.Waliosimama nyuma kutoka kushoto ni Balozi mpya wa Tanzania Uholanzi Wilson Masilingi,Balozi mpya wa Tanzania katika visiwa vya Commoro Chabaka Kilumanga,Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa Geneva Balozi Modest jonathan Mero na Balozi mpya wa Tanzania katika falme za Kiarabu(UAE)Mbarouk Nassor Mbarouk.Kabla ya uteuzi Balozi Liberata Mulamula alikuwa msaidi wa Rais Masuala ya kidiplomasia na aliwahi kuwa katibu mkuu wa nchi za Maziwa Makuu.(picha na Freddy Maro)
Balozi Kilumanga-Commoro Akiapa
Balozi Masilingi-Uholanzi akiapa
No comments:
Post a Comment