Hivi ulikuwa unajua kuna msanii wa bongomovie ilikuwa bado kidogo tu agombee ubunge kwenye jimbo la Ilala, sababu ya kutokugombea ni kwa kukosa kura chache sana za maoni kutoka kwenye chama chake cha CCM akiwa mshindi wa pili kwenye kura za moani. Oky, hapa leo nitakupa wasanii wa bongomovie watatu waliotamka rasmi kwamba mwaka 2015 watagombea ubunge na mmoja wao itakuwa ni mara yake ya pili kukimbika kiti hiki cha ubunge.
1.JUMA CHIKOKA “CHOPA MCHOPANGA”
Mchopanga “Juma Chikoka” baada ya kuchuka fomu 2010
Kama ulikuwa hujui kuhusu huyu jamaa ni kwamba, kama mambo yangemuendea vizuri mwaka 2010. Basi leo hii tungekuwa tunaanza kumuita na neno muheshimiwa, then jinalake lingefuata. Tena siyo wa jimbo la dogo, mbunge wa moja kati ya majimbo makubwa hapa Tanzania jimbo la Ilala. Juma Chikoka akipitia katika chama cha CCM,alifanikiwa kushika nafasi ya pili kwenye kura za maoni akipishana kura chache na mbunge wa Ilala maarufu kama “Zungu”. Unaweza kujiuliza juu ya uwezo binafsi alionao kijana jamaa huyu mkali wa maigizo toka enzi za Kaole kwa kufanikiwa kufika nafasi ya juu kabisa kwenye kura za maoni kugombea jimbo gumu na muhimu kama Ilala.
Chopa mchopanga aliwahi kuwa mwenyekiti wa UVCCM Kinondoni Sharif shamba na baadaye akiwa India alikuwa mmoja kati ya waanzilishi wa tawi la CCM India lililozinduliwa na Mhe. Samwel Sitta.Chopa mwenye anaweka wazi kwamba mwaka 2015 lazima aendeleze harakati kwasababu yeye ni kiongozi makini na mpenda mabadiliko. Kama ulikuwa hujui kitu kingine kuhusu Chopa ni kwamba jamaa alimaliza form six pale Tambaza. Baada ya hapo alipata nafasi ya scholarship kwenda kusoma India baada ya kufaulu vizuri na kipaji chake cha kuigiza kikimuongezea credit za kupata hiyo scholarship. Choka amamemaliza degree yake ya kwanza kwenye chuo cha Bangalore akisomea mambo ya sanaa na mahusiano na jamii(PR). Tumeombee uhai,afya njema na hali hii hii aliyonayo sasa ili 2015 tupate mheshimiwa mwingine kutoka kwenye sanaa,
2.JACOB STEVEN “JB”
Bonge la bwana, kaka mkuu wa tasnia ya bongomovie na yeye pia ni mmoja kati ya wasanii ambao wanatarajiwa kugombea ubunge ikifka 2015. Bado hajaweka wazi atagombea jimbo gani au kupitia chama gani?. Mwaka huu kwa wasanii wa bongomovie yeye ndiyo alikuwa wa kwanza kutangaza nia yake ya kugombea ubunge thou vyanzo vyote vya habari bado havijapata kujua ni jimbo gani ambalo “DJ Ben” ataenda kumwaga sera zake ili mwananchi wamchague ikiwa ni baada ya kupita kwenye kura za maoni kwanza. Imagine that, JB yupo ndani ya mjengo..suti kali na kaenea kwenye kiti chote cha bungeni. Hapo sasa ndiyo zipambe moto harakati za kupambana juu ya piracy kwenye kazi za wasanii. Kama Chopa,..tunamtakia afya njema JB na nia yake isibadilike hadi siku ya uchaguzi ikifika ili tumchague awe mbunge wetu.
3. DEOGRATIOUS SHIJA
Moja kati ya ma-best wakubwa wa marehemu Sajuki, anaitwa Shija. Kwa upande wake yeye ameweka wazi jinsi atakavyogombani ubunge wake na lengo kuu la kugombania huo ubunge.Shija yeye anasema kwamba kutokana na mabadiliko ya katiba yanayoendelea..ni kwamba ana nafasi ya kugombania ubunge akiwa kama mgombea binafsi. Akiongeza infoz zaidi anasema kwamba lengo lake kuwa mbunge ni kutetea haki za wanyama baada ya kujifunza vitu hivyo akiwa Kenya na Uingereza.”Wanyama ni sehemu ya maisha yetu na viumbe kama sisi, sio kila mbunge aingie bungeni kutetea jimbo lake tu bali kuna vitu vingi vinaitaji uwakilishi pia”. Duh! Haya sasa, kitu 2015 hiyo mgombea binafsi Shija na sera yake ni kutetea wanyama. Uhai na afya juu uwe naye ili 2015 afanye kweli.
CHANZO: Bongo movie
No comments:
Post a Comment