Thursday 27 June 2013

FAMILIA YA MANDELA YAKOSOA WANAHABARI

Mtoto mkubwa wa Nelson Mandela,Makaziwe Mandela
Taarifa kutoka Ikulu ya Afrika Kusini zinasema kuwa hali ya kiafya ya rais mstaafu Nelson Mandela sio nzuri na kuwa imezorota katika saa 48 zilizopita.
Baada ya kumtembelea hospitalini, mwanawe mkubwa wa kike Makaziwa, alisema hali inaonekana kuwa mbaya lakini akaongeza kuwa Mandela anaweza kuwasikia jamaa zake wanapomuita huku akijaribu kufungua macho yake.



Wamevuka mipaka ya maadili. Wakati hayati Margaret Thatcher alipokuwa mgonjwa mbona sikuona, ukaribu wa vyombo vya habari kiasi ninachokiona kwa baba yangu? Ni kwa sababu hii ni nchi ya kiafrika. wanahisi kuwa hapa wanaweza kuvuka mipaka wanavyotaka, '' alisema Makaziwe amesema “Nimekasirishwa sana. Kwa sababu Mandela ni kiongozi mashuhuri duniani, haimaanishi utu wake udhalilishwe pamoja na kuvuka mipaka kuingilia mambo yake binafsi Hapa naona kuna ubaguzi wa rangi, huku vyombo vingi vya kimataifa vikivuka mipaka, ni kama ndega aina ya Tai au Vulture wanaosubiri Simba kumla mnyama aliomuwinda kisha wakimbilie mzoga.

CHANZO: BBC

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...