Tuesday 25 June 2013

MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM ALEX ROBERT YUPO HAI!


Alex Robert
Nilikuwa nikisikiliza East Africa radio muda mfupi uliopita na kusikia habari za kuthibitisha kuwa mwanafunzi Alex Robert yupo hai na hajafariki kama ilivyoripotiwa katika mitandao.Nilisikiliza mahojiano kati ya mtangazaji wa East Africa radio na rafiki wa Alex ambaye alikuwepo katika tukio la uporaji na vilevile mahojiano na baba mzazi wa Robert ambaye yupo Dar akitokea Bukoba. Alex amelazwa katika hospitali ya Muhimbili katika chumba cha wagonjwa mahututi na anaendelea vizuri.Tuzidi kumwombea Alex apate nafuu haraka.
imeandikwa na 
Anna Nindi

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...