Vs
Jumamosi ya tarehe 8 juni ndiyo fainali za mashindano ya wazi ya tenisi ya Ufaransa maarufu kama Roland Garros.Mchezaji namba moja wa tenisi duniani Serena Williams atapambana na mchezaji namba tatu,Maria Sharapova.Utakuwa ni mchezo mzuri na wa kusisimua kwani kila mmoja ana ari ya kuchukua kombe.Serena Williams anataka kuendelea kuvunja rekodi kwa kutwaa kombe la 16(grand slam) na Maria Sharapova ndiye aliyetwaa kombe hilo mwaka jana na ni dhahiri anataka alipate na mwaka huu.
Msomaji wetu,je wewe unadhani nani atatwaa kombe hilo?Toa maoni yako tafadhali.
No comments:
Post a Comment