Thursday 27 June 2013

SEHEMU YA 2:RISITI NI HALALI KWA MNUNUZI AU NI MATWAKWA YA MUUZAJI?

Mimi nina utaratibu wa kuweka kumbukumbu za manunuzi yote ninayofanya.Vilevile nchini Sweden ambapo ninaishi unaponunua chochote hupewa risiti hata kama ni ndizi moja.Huombi risiti bali unapewa kama haki yako mnunuzi.Kaka yangu alisema angeifuata siku ya pili kwani kwa siku ile muda wa kufunga duka ulikuwa umepita tayari.
Siku ya pili alikwenda dukani na wakawa wanampa majibu yasiyoeleweka kuashiria kuwa hawatoi risiti.Akanipigia simu kunipa taarifa na mimi nikamwambia nitakutana nae dukani baada ya muda mfupi.Baada ya muda nikawa nimefika dukani.
Bahati nzuri walinikumbuka maana nilikwenda na kaka yangu siku iliyopita.Dukani pale walikuwepo wauzaji wawili.Mimi sikuwa na swala lingine zaidi ya kuwaomba risiti yangu.


Wakaanza kutaka kunizungusha na mimi.Niliwaambia kitu kimoja tu kuwa ``nipeni risiti yangu niondoke kwa amani,nikiondoka hapa bila risiti basi mjue duka hili litafungwa kwani mnaiibia serikali.``
Ukweli waliogopa sana na wakaanza kupigiana simu wahusika.
Naona wakaambiwa wanipe risiti.Nikapewa risiti yangu!
Unajua nini,VAT ya manunuzi niliyofanya ilikuwa 147,000/-!
Hizo ni pesa ambazo wasingepeleka serikalini bali wangeingiza kwenye mifuko yao.Nikawaambia mimi ninajua haki ya mnunuzi ni ipi na ninajua kwanini hawataki kutoa risiti kwa watu kwasababu wanaiibia serikali.Ila pale nilikuwa nazungumza kwa niaba yangu mwenyewe na sikumzungumzia mtu kwa kuwa mimi ndiye nilitoa pesa za manunuzi yale yaliyofanywa.Kitu cha ajabu ,baadhi ya wateja waliokuwepo dukani pale walionekana kunishangaa kabisa masikini.
Wengine wakawa wanasema wao hawajui nini maana ya risiti.Nilichojifunza pale ni kuwa wananchi wanahitaji kuelimishwa.Mamlaka ya mapato wakitoa elimu nzuri kwa wananchi ujanjaujanja kama huu utakwisha.
Wafanyabiashara wengi huogopa watu wanaoelewa sheria na haki zao.Wananchi wanatakiwa kujua kuwa risiti wanapofanya manunuzi ni HAKI yao.
Watu tunailaumu serikali kwa kukosa madawati katika mashule,vitanda vya kutosha mahospitalini n.k.Serikali inaweza kufanya hayo yote kama kodi italipwa kihalali na kwenda mahali panapohusika ili kufanya shughuli za maendeleo.Nchi zote zilizoendelea duniani,kodi inakusanywa na inafanya shughuli za maendeleo ikiwemo kuboresha afya,elimu,ustawi wa jamii nk.
Hivyo mwananchi dai risiti kila unapofanya manunuzi kwa maendeleo ya nchi yako.

Imeandikwa na

Anna Nindi

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...