Stanbic Bank,Tanzania Mwandishi Wetu, Mwananchi
Dar es Salaam. Benki ya Stanbic Tanzania imetajwa kuwa benki bora zaidi kwa utoaji huduma kwa wateja nchini.
Kwa mujibu wa ripoti ya utafiti uliofanywa hivi karibuni uliotolewa na Kampuni ya Ukaguzi wa Hesabu na Ushauri ya KPMG, benki hiyo inaonyesha kutoa huduma bora kwa wateja.
Utafiti huo ulijumuisha benki 32 za Tanzania, huku benki hiyo ikiibuka mshindi wa jumla.
Akizungumza utafiti huo jana, Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa Stanbic Tanzania, Abdallah Singano, alisema benki yake imejikita katika utoaji huduma za pekee za benki na kuwafikia wananchi wasiopata huduma hiyo.
“Tuna furaha kuwa benki bora zaidi inayojikita katika utoaji huduma kwa wateja nchini. Mafanikio yetu yanachangiwa zaidi na uelewa nzuri tulionao juu ya soko hili, teknolojia tunayotumia na kujituma kwa wafanyakazi wetu,” alisema Singano.
Singano alisema benki hiyo ipo kwenye mchakato wa kujiimarisha zaidi, ili iwe injini ya maendeleo ya uchumi kwa sekta muhimu za maendeleo nchini.
|
Monday, 24 June 2013
STANBIC AONGOZA UTOAJI HUDUMA BORA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
PALM TREES ARE BEAUTIFUL
Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...
-
Dar es Salaam: Mwekezaji Sheikh Salim Abdullah ametangaza kuwekeza kwenye Uwanja Wa Ndege wa Kimataifa wa JK Nyerere Dar es Salaam (JN...
-
1. PASTA Hiki ni chakula cha haraka.Unaweza kutayarisha pasta kwa kuongeza tu protini ulizonazo katika jokofu lako mfano kuku...
-
No 10 : Oriens By Van Cleef & Arpels No 9 : Love Sweet Love By Philosophy Love Sweet Love by Philosophy is an ideal summer perfum...
No comments:
Post a Comment