Tuesday 25 June 2013

Tanzania yapata heshima ya kimataifa nchini Ujerumani baada ya kuzindua Viunga vilivyopewa jina la Dar Es Salaam.

Jiji letu la Dar es Salaam limepata heshima ya kimataifa, katika nchi ya Ujerumani kwenye Jiji la Hamburg, Kuna sehemu imepewa jina la Dar Es Salaam Platz ( Dar es Salaam square ).
1 . Picture number ONE
 Kutoka kulia : Brighton Monyo ( Zimamoto DSM ), Bw. Wilson M. Kabwe ( Mkurugenzi wa Jiji DSM ), Mh. Christopher H. Mvula ( Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani ), Godwin D. Msigwa, Bw. Ali Siwa, Bw. Philip H. Mwakyusa wakati wa Uzinduzi wa Viunga vilivyopewa jina la Dar Es Salaam.
2 . Picture number TWO
 Mh. Dr. Didas Masaburi ( Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam ) akipata maelezo kutoka kwa wenyeji wa Jiji la Hamburg akiwa katika sehemu ya Dar es Salaam.


3 . Picture number THREE . Watanzania waioko Ujerumani kwa kubadilishana Ujuzi na Mafunzo
Kutoka kulia : Moses Haule, Godwin Msigwa, Ully Mbuluko, Godfrey Matola na Brighton Monyo ( Watanzania waliopelekwa kwa Mafunzo mjini Hamburg ) wakiwa chini ya kibao kinachoonyesha ile sehemu ya Dar es Salaam jijini Hamburg.
4 . Picture number FOUR . Kiunga kilichopewa jina la DSM
 Huo ndio muenekano wa sehemu ( Dar es Salaam square ) Jijini Hamburg, hapo kuna viunga na kivuli ambapo watu mbali mbali wakati wa tofauti hufika na kupumzika, kusoma vitabu, kukutana na marafiki nk.
5 . Picture number FIVE . Mkurugenzi wa Jiji DSM na Kaimu Balozi wakifaidi kivuli katika DSM square
 Viongozi wa Tanzania wakiwa chini ya kivuli wakati wakisubiri ufuguzi hafla ya ufunguzi wa viunga vya sehemu ya Dar es Salaam Platz ( Dar es Salaam Square ).
Hizo ni baadhi ya picha katika tukio la ufunguzi wa sehemu hii ambayo ni sehemu ya katikati ya Jiji la Hamburg, kwa Dar es Salaam waweza kusema POSTA.

CHANZO: MO blog

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...