Thursday 27 June 2013

WAZIRI MEMBE AMPOKEA MAKAMU WA RAIS WA BOTSWANA



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) (wa kwanza kulia) akiwa na Mwakilishi wa Heshima wa Botswana nchini Tanzania, Bw. Emmanuel Ole-Naiko (wa pili kushoto)  kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere walipokuwa wakimsubiri Makamu wa Rais wa Botswana, Mhe. Ponatshego Kedikilwe kuwasili nchini. Mhe. Kedikilwe ni miongoni mwa viongozi watakaohudhuria Mkutano wa Majadiliano kwa Manufaa ya Wote (Global 2013 Smart Partnership Dialogue) utakaofanyika kuanzia tarehe 28 Juni had 01 Julai, 2013.
Mhe. Kedikilwe akiteremka kwenye ndege mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Mhe. Membe akimkaribisha nchini Mhe. Kedikilwe mara baada ya kuwasili.
Mhe. Kedikilwe akikagua Gwaride la Heshima.
Mhe. Kedikilwe na Mhe. Membe wakifurahia burudani iliyokuwepo uwanjani hapo kwa mapokezi.
Mazungumzo yakiendelea.

CHANZO: Issa Michuzi

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...