Wednesday 26 June 2013

Zanzibar yadhimisha siku ya Upigaji Vita madawa ya Kulevya

01

Waziri wa Afya  Juma  Nuni  Haji akipokea mandamano  yaliongozwa  na vijana wa Chipkizi, katika madhimisho ya siku ya upigaji vita matumizi na biashara haramu ya madawa ya kulevya Duniani huko  Meya , nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
02
Kundi la watu W=walioacha kutumia madawa ya kulevya wakipita kwa mandamano mbele ya mgeni rasmin  Waziri wa Afya  Juma  Nuni  hayupo pichani, katika madhimisho ya siku ya upigaji vita matumizi na biashara haramu ya madawa ya kulevya Duniani.


03
Addy Amer alieacha kutumia madawa ya kulevya akitoa ushuhuda wa madawa ya kulevya, na kuwataka vijana wasijaribi kuyatumia kwani yanahatarisha maisha kwa ujumla.
04
Waziri wa Afya  Juma  Nuni  Haji, akiwahutubia wananchi na waliocha kutumia madawa ya kulevya katika madhimisho ya siku ya upigaji vita matumizi na biashara haramu ya madawa ya kulevya Duniani, kuli Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Tume ya Dawa za kulevya Muhmoud Mussa,kushoto Naibu Kadhi Mkuu Zanzibar Hassan Othman.
05
Waziri wa Afya  Juma  Nuni  Haji akiwa na viongozi mbalimbali, Makanda wa Polisi katika picha ya pamoja na walioacha kutumia madawa ya kulevya huko Meya katika madhimisho ya siku ya upigaji vita matumizi na biashara haramu ya madawa ya kulevya Duniani Jun 26.(Picha na Makame Mshenga- Maelezo Zanzibar).

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...