Saturday, 13 July 2013

BILIONEA WA MAREKANI AINUNUA FULHAM

Bilionea wa kimarekani, Shahid Khan anayemiliki timu ya NFL ya Marekani amenunua timu ya Fulham inayoshiriki ligi kuu ya England. (HM)

TAJIRI Mohamed Al Fayed amethibitisha kuiuza klabu ya Fulham kwa bilionea wa Kimarekani, Shahid Khan, ambaye tayari anamiliki timu ya NFL, Jacksonville Jaguars.
Uhamishwaji umethibitishwa na Ligi Kuu ya England. Khan anamiliki asilimia 100 ya hisa za klabu sasa na hakuna deni. Tangazo rasmi lilitarajiwa kutolewa saa 7 jana Craven Cottage.
"Wakati wa kuwa mmiliki wa Fulham Football Club siku moja utafika mwisho, na nafikiri wakati huo sasa umefika,"alisema Al Fayed.


"Wakati ni mwafaka kwa sababu nimempata mtu mzuri sana wa kuichukua, Shahid Khan amekubali kupokea majukumu na kipaumbele ambacho nimekuwa nacho Fulham tangu mwaka 1997. 
"Fulham itakuwa katika mikono mizuri sana na Shahid, ambaye ni mfanyabiashara mwenye mafanikio na mwenye mapenzi na michezo kwa kila ushahidi. Naomba kila mmoja anayependa Fulham na Uwanja wetu wa nyumbani wa Craven Cottage kumkaribisha Shahid kuanza safari yake ya kuwa mlezi mpya wa Fulham Football Club,"alisema.
  Khan alisema:  "Nimekuwa mwenye bahati sana hivi karibuni, kutambulishwa na Mohamed Al Fayed, mtu ninayemuheshimu na kumzimikia kwa mambo aliyoyafanya katika maisha yake na - juu ya yote, kwa aliyowafanyia wengine,"
Chanzo: binzubeiry

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...