Stori:Dustan Shekidele,Morogoro
MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera juzikati alionyesha wananchi wake umahiri mkubwa wa kuucheza muziki mtindo wa Kwaito huku akiwafunika vibaya vigogo wa Benki ya NMB Mkoa wa Morogoro waliokuwa wakicheza naye.

Bendera alionyesha umahiri huo ndani ya Ukumbi wa Hoteli ya Kitalii ya Morogoro kwenye sherehe kabambe ya kumuaga aliyekuwa Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Wami aliyefahamika kwa jina moja tu la Bushiri aliyehamishiwa Wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro ambapo mkuu wa mkoa alisakata Kwaito kwa mbwembwe nyingi.
“Hakika Bendera ni mwanamichezo, kumbe siyo kwenye soka tu bali hata kwenye dansi yumo, umeona pale ni kama wanashindanishwa lakini kama ni ushindi basi angepewa yeye,” alisikika akisema mwalikwa mmoja aliyejitambulisha kwa jina na John Sheki.
Licha ya kuwa mwanasiasa na kuonesha umahiri wa kucheza dansi, Bendera aliwahi kuwa Kocha wa Timu ya Taifa, Taifa Stars mwaka 1983 hadi 1986 na akawa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mpira wa Miguu (FAT) mwaka1978 hadi 1979.
Sherehe hiyo iliyofana ilihudhuriwa na wafanyakazi wa matawi yote ya NMB Mkoa wa Morogoro na baadhi ya wateja wa benki hiyo ambao walikuwa wageni waalikwa na ilianza saa 2 usiku ikafika tamati saa 6 usiku huku gumzo likiwa ni usakataji wa Kwaito wa Bendera.

CHANZO: GPL
No comments:
Post a Comment