Wagonjwa wa figo wapatao sabini wako katika hali mbaya na maumivu makali kutokana na asilimia kubwa yao kukiri kushindwa kumudu gharama za matibabu ya ugonjwa huo kutokana na ukosefu wa fedha unaochangiwa na hali duni ya maisha.
Kutokana na matatizo ya wagonjwa hao,ITV iliwatembelea na kukuta baadhi yao wakiwa katika chumba maalum cha wagonjwa wa figo katika hospitali ya Regency ya jijini Dar es Salaam wakiwa wamewekewa mashine inayosaidia kusafisha damu ambayo ni gharama kubwa,ambapo baadhi ya wagonjwa walieleza kukata tamaa kutokana na maisha yao kuwa hatarini baada ya kukosa fedha hivyo kuomba kusaidiwa ili waende nje kuwekea figo mpya kupitia account Tanzania kidney patients foundation-crdb azikiwe premier namba.
Daktari anayewahudumia wagonjwa hao bwana Blasius Mlelwa, ameeleza namna wagonjwa wanavyohangaika,huku mmiliki wa hospitali hiyo dakta Rajni Kanabar akikiri kushusha gharama za matibabu kwa wagonjwa wa figo katika hospitali yake lakini asilimia kubwa ya wagonjwa bado hawana uwezo kabisa kumudu matibabu na hasa ya kwenda nje ya nchi.
ITV iliamua kufika wizara ya afya na ustawi wa jamii kwa lengo la kujua mikakati ya serikali katika kusaidia wagonjwa hao,ambapo mkurugenzi wa tiba dakta Margaret Mhando, amesema serikali ina nia thabiti ya kusaidia na mara nyingi inatoa nafasi ya kwanza kwa wagonjwa wa figo,moyo na saratani katika kuwasafirisha kwenda nje kwa matibabu licha ya kuwepo kwa uhaba wa fedha kwa kupeleka wagonjwa wengi,lakini mgonjwa ni sharti akafika kwanza katika hospitali za serikali za rufaa kama Muhimbili, Moi, Ocean road na Bugando ili kuonana na madaktari ili kusaidia kama anavyofafanua hapa.
No comments:
Post a Comment