Tuesday 10 September 2013

Mfumo mpya malipo ya ada waleta neema TRA


Dar es Salaam. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imekusanya zaidi ya Sh4.7 bilioni, baada ya kuanzisha mfumo mpya wa kulipia ada za magari kwa njia ya mtandao.
Kiasi hicho kimekusanywa ndani ya wiki tatu tangu kuanza kwa mpango huo na kimeelezwa kuwa ni ongezeko la Sh1.1 bilioni ya kiasi cha fedha zilizokuwa zikikusanywa katika kipindi kama hicho mwaka jana.
Imeelezwa kuwa katika kipindi cha mwaka jana kabla ya kuanzishwa kwa utaratibu huo, TRA ilikusanya Sh3.6 bilioni.

Akizungumza na gazeti hili jana, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi katika TRA, Richard Kayombo, alisema mfumo huo umesaidia kuondoa msongamano katika ofisi za mamlaka na kuepusha udanganyifu uliokuwa ukifanywa na vishoka.
“Kulikuwa na utapeli mwingi uliokuwa unafanywa na baadhi ya watu kwa kushirikiana na baadhi ya watumishi wetu. Kwa hiyo mfumo huu utasaidia kuondoa kero zote hizo,”alisema Kayombo.
Kwa mujibu wa Kayombo, utapeli huo ulisababisha watu kuchelewa kupata huduma na kwamba baadhi ya watu walikuwa na risiti za benki ambazo ni za kughushiwa.
Hata hivyo alisema wale wanaotaka kubadilisha umiliki wa magari, lazima waende ofisini kwa ajili ya uhakiki wa nyaraka.
Mkurugenzi huyo pia alisema wameanzisha mfumo mwingine wa kudhibiti mizigo bandarini.
Alisema mfumo huo ulioanza mwishoni mwa mwezi uliopita unalenga katika kupunguza kero na malalamiko kutoka kwa wadau na kuisaidia Serikali, ili isipoteze mapato.
Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, mfumo huo ulibuniwa kwa ushirikiano na kampuni ya Korea Kusini na maofisa wa TRA.
CHANZO: MWANANCHI

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...