Thursday, 5 September 2013

MKOA KWA MKOA: TEMBELEA MKOA WA TANGA KATIKA PICHA



Mji wa Tanga ni mji mkuu wa Mkoa wa Tanga uliyoko ufukoni mwa Bahari ya Hindi. Tanga ina bandari kubwa kabisa katika sehumu ya kaskazini mwa Tanzania. Njia ya reli kwenda Mji wa Moshi inaanza hapa.
Jina hili la mji wa Tanga lilitokana neno la Kiajemi lenye maana nne tofauti ambazo ni: Iliyo nyooka; Bonde lenye rutuba; Barabara upande wa mto na Shamba juu ya mlima, neno hilohilo la Tanga kwa kabila la Kibondei ambalo ni wenyeji wa mkoa huo linamaana ya shamba, wao hulitamka N'tanga.
Tanga ni mji muhimu kihistoria kufuatia kuwa Pangani ilikuwa pia kituo muhimu cha misafara iliyoanza hapa kuelekea ndani ya bara na pia soko muhimu la watumwa.
 Baada ya Uingereza kuchukua utawala wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani reli ya Tanga-Moshi iliunganishwa na ile ya kati hivyo ikawa na njia kwenda Daressalaam pia.
Mji wa Tanga una vivutio mbalimbali vya utalii kama vile mapango ya Amboni, mbuga za Saadan, magofu ya Tongoni.Tongoni ipo kilomita 20 kusini mwa Tanga na mzunu wa kwanza kutembelea eneo hili alikuwa ni Vasco da Gama mwaka 1498.
Tuanze safari ya kutembelea Tanga katika picha.



Mitaa ya Tanga



Tanga mjini
File:Bombo HospitC.JPG
Jengo la Cliff lililopo katika hospitali ya mkoa ya Bombo.Jengo hili lilijengwa na wajerumani.

Jengo la mahakama ya Mwanzo ya Usambara ambalo lilijengwa na Wajerumani

Hoteli ya Mkonge


Hoteli ya Tanga Beach Resort

Ofisi za Katani Ltd




Jengo la posta

Maktaba ya Tanga




Mitaa ya Tanga
Jengo la Mamlaka ya Bandari Tanga
harbor
Bandari ya Tanga

Jamat,Tanga



Uhuru Park


Magofu ya Tongoni.Haya ni mabaki ya msikiti katika karne ya 15


Mabaki ya nyumba za waarabu,Pangani

The Exit

Mapango ya Amboni ambayo yalikuwa ni maficho ya Osale Otango aliyewasumbua sana wakoloni wa Kijerumani kwa kuwaibia au kuwauwa



Kiwanda cha maziwa,Tanga Fresh ambacho kipo Tanga.Kiwanda hiki kinatengeneza bidhaa mbalimbali kutokana na maziwa kama jibini, maziwa ya mtindi n.k


Wilaya ya Pangani ni maarufu kwa kilimo cha nazi


Wakazi wa Tanga hujishughulisha na uvuvi.Pichani biashara ya samaki katika soko maarufu la samaki lijulikanalo kama Deep Sea
fishermen
Waachuuzi wa samaki


Shamba la mkonge. Mkonge ulikuwa ni zao la biashara Tanga,kwasasa sijui kama unalipa kama ilivyokuwa katika miaka ya nyuma.
Imeandaliwa na Anna Nindi

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...