MWANADASHOSTI anayejipanga kurejea kwenye gemu la Bongo Fleva kwa kishindo, Rehema Chalamila ‘Ray C’ amefunguka ya moyoni akisema kuwa anamshukuru Mungu kwa kupona madhara ya madawa ya kulevya bila kupata matatizo mengine ya kiafya huku akifafanua suala la kuokoka.![](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_uZIoDGkbh4mwVFKvrOlCFFsJ8dLu7NftmM1mmTUlUC-IsczcyzkdDXo1FX-kpqrVyNovR_bxGN9-BU6VUSfpc7SxfzRmr5QB0ZnbX_Y1Vmp5s_lp5WTLYeoCIIF8S6PuLlrG6MWJUCuLrQC76XRKLtnTB9ttUf8UsWCHrN0-lLfmFXcN4Izcnl4Sh5ZnMeEhMuXoML9rlz2Jf0-8RGBIFfSOOE6d2UlDeZFyx5jpgH_OhsfSSn=s0-d)
Mwanamuziki huyo alisema kuwa katika kipindi chote cha kupigana na madawa ya kulevya zaidi ya miaka mitatu iliyopita, alipitia mengi magumu lakini kikubwa ni kwamba hivi karibuni alipima na kujikuta yupo salama na hana Ukimwi.
Kuhusu suala la kuokoka, Ray C alisema ukweli ni kwamba mwanzoni alikuwa Mkatoliki lakini hivi karibuni alibatizwa na maji mengi katika Kanisa la Sloam lililopo Mbezi-Beach na kuungana na mama yake anayesali kwenye kanisa hilo.
CHANZO: GPL
No comments:
Post a Comment