Usain Bolt aainisha mpango wake wa kustaafu baada ya michezo ya olimpiki ya Rio de Janeiro 2016
Bolt anataka kushinda michezo yote ili kuvunja rekodi ya dunia
Mkimbiaji mwenye kasi zaidi duniani Usain Bolt, anatarajia kustaafu rasmi mchezo huo mara baada ya kumalizika kwa michezo ya olimpiki ya Rio de Janeiro 2016. Agosti 21, siku michezo hiyo itakapohitimishwa, atakuwa anatimiza umri wa miaka 30.
Usain Bolt anashikilia rekodi ya dunia ya mbio za mita 100 na mita 200.
HAYA NDIYO MAFANIKIO YA BOLT
OLIMPIKI
Beijing 2008: Medali za dhahabu tatu
London 2012: Medali za dhahabu tatu
BINGWA WA DUNIA
Berlin 2009: Medali za dhahabu tatu
Daegu 2011: Medali za dhahabu mbili
Moscow 2013: Medali za dhahabu tatu
Hivi karibuni,Bolt alishinda medali 3 za dhahabu huko Mosko,Urusi,
Kama Usain Bolt atachukua medali tatu za dhahabu katika michezo ya olimpiki ya Rio mwaka 2016, atakuwa ndiye mchezaji bora wa michezo ya olimpiki kuwahi kutokea.
No comments:
Post a Comment