Thursday 3 October 2013

JE,UNAZIJUA HAKI ZA WATOTO?



  1. Watoto wote wana haki sawa bila kujali rangi zao, jinsia, lugha, dini, siasa au maoni mengine
  2. Mtoto ana haki ya kutokunyanyaswa
  3. Mtoto ana haki ya kuwa na jina na kuwa raia wa nchi
  4. Mtoto  ana haki ya kupewa  huduma maalum na ulinzi , chakula kizuri, makazi na huduma za matibabu.
  5. Mtoto ana haki maalum ya kukua na kuendelea kimwili na kiroho, kiafya  katika njia ya kawaida,kwa uhuru na  utu.
  6. Mtoto ana haki ya upendo na uelewa, kutoka kwa wazazi na familia, na kutoka kwa serikali endapo wazazi na familia wakishindwa kutekeleza hili.
  7. Mtoto ana haki ya kupata elimu bure, kucheza na kupata nafasi sawa kujiendeleza binafsi. Wazazi wanalo jukumu maalum la kuhakikisha mtoto anapata elimu na mwongozo
  8. Mtoto ana haki ya kuwa wa kwanza kupata msaada
  9. Mtoto ana haki ya kulindwa dhidi ya vitendo kikatili au unyonyaji, kwa mfano wewe haitalazimika kufanya kazi ambayo inazuia maendeleo yako  kimwili na kiakili.
  10. Mtoto anapaswa kufundishwa amani, uelewa, kuvumiliana na  urafiki kwa watu wote.


No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...